SIMIYU;MAPYA YAIBUKA WENYE VYETI FEKI.

.Waanza
kuyakimbia madeni waliyokopa,
.Wategemezi
wao wahaha kukosa wasaidizi.
SIKU chache baada ya serikali kutangaza na kuyaweka
hadharani majina ya watumishi wa Umma wenye vyeti feki baadhi yao wameanza
kuyakimbia madeni walikopa kwa watu binafsi, huku wategemezi wao wakikosa
mahali pa kukimbilia.
Kufuatia uchunguzi uliofanywa na waandishi wa Habari
mkoani Simiyu umebaini kuwa baadhi ya watumishi wa umma hasa walimu waliokuwa
wamekopa kwa watu binafsi waeanza kukimbilia kusikojulikana huku baadhi yao
wakizima simu na kuyahama makazi yao kimyakimya.
Mashaka Magembe mmoja wa wafanyabiashara mjini
Bariadi alisema kuwa amekuwa akiwakopesha walimu kwa riba, lakini baada ya
kubaini kuwa baadhi yao wameondolewa katika utumishi wa umma kwa kuwa na vyeti
feki alianza kuwatafuta ili kulipa madeni lakini hakufanikiwa.
‘’baada ya kuyaona majina yao katika orodha ya
watumishi hewa, niliwapigia simu lakini hawakuweza kunipa ushirikiano kama
awali…mmoja nilikuwa namdai laki tatu, nilipompigia simu alisema tukutane
mtaani badala ya nyumbani kwake na nilipofuatilia kwake nikakuta ameshahama’’
alisema Magembe.
Aliongeza kuwa baadhi yao wamerejesha fedha kidogo
huku wakisema kuwa hali imekuwa mbaya kulingana na majina yao kubainika katika
orodha ya watumishi huku wakiahidi kuwasimamishia riba na watakuwa wanalipa
kidogokidogo.
Alisema kuwa Mwalimu mmoja (jina linahifadhiwa) hadi
sasa hajui aliko na simu yake wakati huo ameshahama alipokuwa anaishi ambapo
kwenye mkataba wa mkopo aliweka dhamana ya seti ya kochi, tv, friji na kitanda.
Kwa Joel Peter ambaye ni Mwanafunzi wa chuo cha
Ualimu Tabora alisema kuwa kwa sasa hataweza kumalizia masomo yake kutokana na
wategemezi wake wote kubainika wana vyeti
feki.
Alisema kuwa kaka yake ambaye ni Mwalimu huko
Itilima amebainika ana vyeti feki hivyo amekuwa na wasiwasi juu ya upatikanaji
wa fedha za kumalizia masomo yake ya ualimu.
‘’Japhet Lasphord Katembo na mke wake wote
wamebainika na vyeti feki na ndiyo walikuwa wakinisomesha, sasa sijui itakuwaje
na wazazi wangu walishafariki’’ alisema Joel huku akiiomba serikali kunagalia namna ya kuwasaidia wanafunzi walioko masomoni.
Aidha kufuatia agizo la Rais Magufuli la kuwataka
watumishi wenye vyeti feki kutoonekana maofisini baadhi ya maafisa utumishi
mkoani Simiyu wameanza kuwatumia barua za kufukuzwa kazi kwa watumishi hao mara
moja.
Na mwandishi wa MAKALIBLOG; COSTANTINE MTAHIAS, SIMIYU.