KUELEKEA UCHAGUZI WA MARUDIO SIHA, CHADEMA WAPATA PIGO ZITO
Kilimanjaro. Mchana wa leo Jumapili Januari 28, 2018, taarifa za
kuaminika kutoka katika kata ya Ormelili wilaya ya Siha mkoani
Kilimanjaro zinasema chama cha CHADEMA kimekimbiwa na viongozi wake.
Viongozi wanaodaiwa kukimbia ni kutoka kata ya Ormelili ambao kwa
pamoja wamejiuzulu nafasi zao na kujivua uanachama wa chama hicho, hivyo
kuomba kujiunga na chama cha CCM.
Taarifa zaidi zinasema na aliyekuwa mfadhili wa ofisi za chama katika
kata hiyo Bi. Janneth Mamboleo Mushi nae amekikacha chama hicho na
kujiunga na CCM ambapo pia amechukua nyumba yake na kuwafanya CHADEMA
kukosa ofisi katika kata hiyo.
Viongozi hao wamepokelewa na ndugu Humprey Polepole ambaye ni Katibu
wa Itikadi na Uenezi Taifa, alipokuwa kwenye kampeni za kumnadi mgombea
Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Siha.
Hili ni pigo lingine zito kabisa kwa CHADEMA ambapo ni masaa machache
tu yamepita toka walikuwa madiwani wa viti maalumu kupitia chama hicho
kujiuzulu na kujiunga na CCM huko wilayani Rombo.
SOURCE DARMPYA.