SHIRIKA LA AGPAHI LATOA SEMINA KWA VIONGOZI WAVIU WA SHAURI MKOANI MARA;
Picha ya pamoja ya washiriki wa warsha iliyokuwa ikitolewa na Shirika la AGPAHI mjini Musoma, mkoani mara baada ya kumaliza warsha hiyo
Dr Felix Kivuyo (katikati , shati jeupe) akikabidhi cheti mara baada ya kukamilika warsha ya WAVIU washauri kukamilika.
Mshindi a warsha aliyeshikilia cheti akipongezana na Afisa Huduma unganishi AGPAHI ambaye pia ni mwezeshaji kutoka Geita-Richard Kambarangwe
Dr.Kivuyo akiendelea kukabidhi vyeti kwa washiriki
Jovin Jonathan (afisa huduma unganishi wa AGPAHI mkoa wa Mara) akitoa mada kwenye warsha hiyo
Washiriki wakipitia baadhi ya mada ambazo walipewa kujadiliana
Bonji Bugeni chac kutoka Bunda Tc kushoto kwake ni DR.Kivuyo wakisisitiza umoja kabla ya kutoa vyeti
Bi.Happiness Malamala, MVIU muelimishaji kutoka mkoa wa Simiyu, kushoto kwake akiwa na mwelimishaji mwenzake kutoka mkoa wa shinyanga (Kanzaga Fabian)
Mshiriki akichangia mada katika warsha

Richard kamabarangwe afisa huduma unganishi AGPAHI kutoka Geita akiendelea na mafunzo kwa washiriki wa warsha hiyo
Na MAKALIBLOG.MUSOMA
Shirika la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative ( AGPAHI) linalotoa huduma za Virusi vya Ukimwi na Ukimwi katika mkoa wa Mara limefanya warsha kwa Waviu Washauri wapatao 24 ili kuwajengea kazi wanazozifanya wakiwa kwenye kliniki ya matunzo na matibabu vilevile majumbani.
Warsha hiyo ya siku tatu iliyofanyika katika ukumbi wa BISHOP JOHN RUDIN CONFERENCE CENTRE ulioko katika Manispaa ya Musoma, mkoani Mara ilihusisha wilaya tatu za Bunda mjini, Bunda vijijni na Rorya. Vilevile warsha ilihususha Waviu washauri wawili ambao ni wazoefu na mameshahudhuria warsha kama hii huko nyuma kwa ajili ya kubadilishana uzoefu.
Akizungumza katika semina hiyo, Ofisa unganishi wa AGPAHI kwa mkoa wa Mara Bw. Jovin Jonathan alisema, miongoni mwa vitu ambavyo vilisisitizwa kwenye workshop ni ufuasi mzuri wa dawa kwa wateja vilevile kuwapa matumaini chanya kwa wateja ambao wamekata tamaa ili waendelee kukaa kwenye huduma.
Kwa upande mwingine, Bwana Richard Kambarangwe ambaye ni Afisa huduma unganishi AGPAHI kutoka mkoni Geita na mwezeshaji wa warsha aliwataka WAVIU hao kuendelea kuwa wakweli kwa kuwahimiza wateja wao kufika kwa wakati katika maeneo Kliniki za matunzo na matibabu na akati wauchukuaji dawa.
Aidha baadhi ya wawezeshaji kutoka katika mkoa wa Mara hususani wilaya ya Rorya walisema kuwa kumekuwepo na taarifa baadhi ya wafugaji kutumia dawa za kufubaza VVU / kunenepesha kwa mifugo yao hivyo waliitaka serikali kufatilia kwakina nakuwachukulua hatua wanao husika.
Akifunga warsha hiyo kwa niamba ya Mganga Mkuu wa Mkoa Mara, Dr Felix Kivuyo aliwataka waviu hao kuzingatia utumiaji sahihi wa dawa na maisha yataendelea vyema huku akiwataka waelimishaji kwenda kuwasimamia vyema wateja wao.
Dr. Kivuyo amewataka waviu ambao ni viongozi katika maeneo mbalimbali kuhakikisha wanawashauri wateja vyema na kusisitiza kuacha kutoroka kwenye huduma. Kuwarudisha wateja kwenye huduma na kuhakikisha wanaendelea kupata dawa. “Ndugu zangu mkizingatia utumiaji mzuri wa dawa haitakuwa shida kwahiyo tuwe makini sana na tunatakiwa kuwafata wagonjwa wengine ambao wako mitaani”.
Aidha Dr. Kivuyo alisema kuwa dhamira ya serikali ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2030 hakuna maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi.