Jambazi Auwawa na Wananchi WAakati Akiwatoroka Askari
Jambazi mmoja ameuawa na wananchi wakati akiwatoroka askari baada ya kubainika kufanya jaribio la kutenda uhalifu katika mradi wa ujenzi wa kituo cha pamoja cha forodha OSBP Tunduma Mkoani Songwe.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi kamishna msaisizi wa polisi Mkoani wa Songwe amesema tarehe 10 usiku wa kuamkia jumatano hii majambazi hao walipanga kufanya tukio la uhalifu katika mradi wa ujenzi wa kituo cha forodha OSBPTunduma na kwamba baada
tarehe 10 usiku wa kuamkia
jumatano hii majambazi hao
walipanga kufanya tukio la
uhalifu katika mradi wa
ujenzi wa kituo cha forodha
OSBPTunduma na kwamba baada
ya kugundulika walikimbia na
kutelekeza bunduki yenye risasi
30, na zana zingine walizokuwa
nazo.Kamanda Nyange amesema
majambazi wawili walifanikiwa
kutoroka wakati mmoja
aliyetajwa kwa jina la Isha
Martin Mwampulo (20) mkazi
wa Lwasho kata ya Ndalambo
wilayani Momba akinaswa na
wananchi, ambapo hata hivyo
baada ya kushambuliwa alijeruhiwa
vibaya na kufariki dunia akiwa
njiani kuwahishwa hospitali.
Wakazi wa mji wa Tunduma
mbali ya kupongeza jitihada
za jeshi la polisi, wamesema
wako tayari kushiriki kikamilifu
katika kufichua wahalifu
lakini wakataja kasoro ya
askari kuchelewa kufika
pindi wanapoarifiwa kuhusu
uhalifu jambo linalowakatisha
tamaa wananchi katika
kushiriki kupambana na uhalifu.
Aidha jeshi la polisi limedai
kuwa jambazi huyo alikuwa
amevaa sare za wakandarasi
na kutumia mwanya huo
kutaka kutekeleza azma yake.
Kamanda nyange ameendelea
kutahadharisha kuwa Mkoa
wa S ongwe sio mahali
salama kwa wahalifu na
kupongeza ushirikiano wa
wananchi kwa jeshi la polisi
hadi hivi sasa .
source saut yakwetu.