: BEKI ALIYEMPIGA KIWIKO MARTIN AFUNGIWA MECHI TATU


Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imemsimisha beki wa Majimaji, Juma Salamba mechi tatu za Ligi Kuu Bara.
Taarifa zinaeleza Salamba amefungiwa mechi tatu kutokana na kitendo cha kumpiga kiwiko kiungo wa Yanga, Emmanuel Martin.

Salamba amepatikana na hatia baada ya tukio hilo la kumpiga kiwiko Martin katika mechi ambayo iliisha kwa sare ya 1-1 kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Powered by Blogger.