KOCHA WA BIASHARA UNITED ATUMA SALAM KWA DODOMA FC;
![]() |
Mwalimu wa timu hiyo Ya Biashara United amesema hawahofii Dodoma fc ambapo ameahidi kuendelea na kuvuna pointi tatu katika uwanja wa nyumbani.
Nimechi ya pili kwa Biashara United hii katika ligi hiyo kutokana na ushindi ambao waliupata kutoka kwa Toto africani ya mwanza ambapo sasa watakipiga na Dodoma fc ambao nayo inafundishwa na jamhuri Julio kiwelu.
Akizungumza na Makaliblog mwalimu wa timu hiyo kuelekea katika mchezo wa kesho Aman Josiah amesema wachezaji wote wako katika morali kuelekea mechi hiyo ambayo itapigwa jumamosi hiii katika uwanja wa kumbukumbu ya karume.
Amani alisema kuwa katika mchezo wa kesho watahitaji kuwa na maendeleo mazuri kutoka mechi ya kwanza hadi ambayo watacheza jumamosi hiii ili kujiweka katika nafasi nzuri zaidi.
“Ukiangalia kwenye michezo hii ya kwanza hakuna timu ambayo ili pata magori zaidi ya mmoja ambapo utaona jinsi gani kundi letu nigumua”.alisema aman
Mwalimu alisema anamatumaini makubwa kutokana na wachezaji wa Biashara kuwa fiti isipokuwa mchezaji mmoja ambae ni Nahodha wa timu hiyo Forume ambaye anasumbuliwa na madonda ya tumbo lakini alisema kufikia kesho wataangalia kama anaweza kushiriki katika mchezo wakesho.
Hivyo aliwataka wanamara kuendea kuiunga mkono timu yao kwani wataendelea kuvuna pointi tatu na amewataka mashabiki kuwa na umoja na Timu yao ili kuwa nyuma ya timu kwani watashiriki kwa nguvu zao zote katika mchezo huuo.
Biashara united niya pili katika msimamo wa kundi “C” ambapo kundi hilo linaoongozwa na Alliance school. Kundi hilo lina timu nane ambapo lina Allianced school,Biashara Mara,Dodoma Fc,Jkt OLjoro,Transi Camp,pamba Sc,Rhino Rangers na Toto Africans.