AJIBU AREJESHWA STARS;


Na mwandishi wetu
KIUNGO mshambuliaji wa timu ya Yanga Ibrahim Ajib amejumuishwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinachojiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi ‘The Flames’ mwezi ujao.

Stars itaingia kambini Oktoba mosi kwa ajili ya mchezo huo utakaopigwa wiki moja mbele katika uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Ajib kuitwa na kocha Salum Mayanga tangu ajiunge na Yanga akitokea Simba mwezi Julai mwaka huu.

Katika kikosi hicho chenye wachezaji 21 kiraka Erasto Nyoni ameendelea kuaminiwa akiwa amedumu kwa miaka 10 mpaka sasa ndani ya Stars.
 
KIKOSI KAMILI CHA STARS HICHO HAPO CHINI
Makipa ni Aishi Manula, Peter Manyika na Ramadhan Kabwili. Walinzi ni Boniface Maganga, Abdi Banda, Gadiel Michael, Kelvin Yondan, Salim Mbonde, Nyoni na Adeyun Salehe.

Viungo ni Himid Mao, Hamis Abdallah, Mzamiru Yassin, Raphael Daud, Simon Msuva, Shiza Kichuya, Ajib, Morel Ergenes na Abdul Hilal.

Kocha Mayanga ameita washambuliaji wawili tu ambao ni nahodha Mbwana Samatta na Mbaraka Yusuph.
Powered by Blogger.