TCRA,WAJA NA HUDUMA TOKA MTANDAO MMOJA KWENDA MTANDAO MWINGINE BILA KUBADILI NAMBA YAKO YA SIMU;



Mwesigwa Felcian mhandisi wa mawasiliano akitoa mafunzo kwa wanandishi wa habari mkoani mara




mwandishi wa habari kutoka kituo cha CLAUDS media Musoma akifatiria mada katika mafunzo hayo.



Thadayo Ringo Naibu Ded masuala ya utumiaji huduma na bidhaa mawasiliano akitoa maelezo katika mafunzo hayo na wandishi wa habari



aliye valia tshet nyeupe ni mmiliki wa Makaliblog akifatiria mjadala

sehemu ya wana habari wa vyombo mbalimbali mkoani mara.




picha na Makaliblog
MAMLAKA ya mawasiliano nchini TCRA imewaomba wakazi wa mkoa wa Mara kutumia mfumo mpya ya mawasiliano utakao muwezesha mtumiaji wa simu ya kiganjani kuhama kwa hiari toka mtandao mmoja wa simu kwenda mtandao mwingine bila kubadili namba yake
Huduma hiyo ya kisasa itatolewa kwa mtumiaji wa simu hiyo ambaye hajaridhishwa na huduma aliyokuwa akiipata katika mtandao anaouhama njia ambayo itamtaka kubaki na namba yake ileile itakayo kuwa ni kitambulisho chake mahali kokote atakapohamia watu watampata bila hata kuwataarifu marafiki,familia na wafanyakazi wenzake

Kauli hiyo ilitolewa Jana na mhandisi mwandamizi wa mamlaka hiyo Mwesigwa Felician alipokuwa akifanya utambulisho wa Huduma hiyo kwa waandishi wa habari mkoani hapa, alisema mfumo huo unafahamika kwa lugha ya kingereza kuwa ni Mobile Number Portabilty(MNP) yaani huduma ya hiari na yenye uhuru.

"Mtoa huduma wako wa awali hatakiwi kukushawishi kwa namna yoyote ile ili ubaki wakati wa kuhama akifanya hivyo toa taarifa kwa mtoa huduma unapohamia au TCRA, ila unawaeza kuhairisha kuhama kwa hiari yako mwenyewe, kabla ya kutuma ujumbe wa HAMA kwenda 15080"alisema Felician.

Kwa upande wake naibu mkurugenzi wa masuala ya watumiaji Thadayo Ringo alisema Huduma hiyo ilianza kutumika nchini machi mosi mwaka huu sambamba na hilo inapatikana wakati maduka, ofisi na maeneo ya mauzo ya mtoa Huduma mpya vinapokuwa vimefunguliwa kwa Wateja.


Alisema ili mtumiaji wa huduma hii ya MNP aweze kufurahia Huduma za kibenki kupitia mtandao ya simu(mobile Banking) kwakuwa atapewa laini mpya itamtaka kuwasiliana kwanza na tawi la benki kuhama kwasababu amehamia mtandao mwingine ili aunganishwe upya na Huduma hizo.

"Wateja walio kwenye mfumo wa kulipia Huduma kabla ya matumizi hawataweza kuhama na salio na watatakiwa kutumia salio ili kabla ya kuhamia kwa mtoa Huduma mwingine la sivyo Salio lake litapotea pia hairusiwi kuhama kama unadeni lolote alisema.

Ringo aliongeza kuwa mfumo huo wa mawasiliano tayari umekwisha anza kutumika katika baadhi ya nchi za bara la Afrika zikiwemo nchi za Afrika kusini na Nigeria.
Powered by Blogger.