NDANDA: Tuna hasira, ATAKAYE KUJA NANGWANDA HALALI YETU;


BAADA ya kucheza mechi tatu za ligi ugenini wakifanikiwa kushinda moja, sare na kufungwa moja Ndanda FC wanarejea Nangwanda Sijaona wakitamba wanaenda kuanza kutoa dozi kwa kila atakayegusa uwanja huo wakijivunia timu yao kupata muunganiko mzuri.

Ndanda iliyoondokewa na baadhi ya nyota wake msimu huu kama nahodha Kigi Makasi aliyejiunga na Singida United na kiungo Rifat Hamis aliyehamia Mtibwa Sugar ilikuwa ikidhaniwa itafanya vibaya kwenye ligi lakini hali imekuwa tofauti baada ya kuonyesha uwezo wa kuridhisha na kufanikiwa kupata pointi nne katika mechi tatu za ugenini.

Kocha msaidizi wa Ndanda, Musa Mbaya amesema baada ya kukubali kipigo cha bao moja kutoka kwa Yanga jana wanarejea nyumbani ambapo watacheza mechi tatu na wana matumaini makubwa ya kufanya vizuri.

“Timu inarejea Mtwara sasa, ni matumaini yetu tutatumia vizuri uwanja wa Nagwanda kupata matokeo katika mechi zetu tatu zinazokuja, wachezaji wetu wameanza kuelewana na timu inapata muunganiko mzuri,” alisema Mbaya.

Akizungumza kuhusu mchezo wa jana dhidi ya Yanga, Mbaya alisema kukosa umakini kwa wachezaji wake kulipelekea kipigo hicho lakini waliweza kuwadhibiti vizuri nyota wa mabingwa hao.

“Tulitengeneza nafasi kadhaa, tuliwazuia vizuri Yanga ila tumefanya kosa moja wamelitumia tukakosa pointi tatu tunarudi Nangwanda kujipanga,” alimaliza Mbaya.
Powered by Blogger.