Mtu mmoja amefariki dunia baada ya kujigonga kwenye gari ya polisi baada ya kupata kiwewe alipoona gari hiyo ambapo alikuwa amebeba samaki na kufariki papohapo.
Tukio hilo limetokea katika kijiji cha ingri juu huko shirati wilayani Rorya mkoani mara nakusababisha kifo cha kijana huyo mwenye umri wa miaka kumi na saba mfanya biashara wa samaki namkazi wa Ingri juu. Inadaiwa kuwa marehemu alikuwa anapeleka samaki ndipo alipokutana na gari ya polisi ikiwa imefunguliwa milango nakujingonga na kupoteza maisha papohapo. Kutokana na kuwepo kwa tarifa kuwa gari la polisi ndio chanzo cha kifo hicho shuhuda huyo amesema kuwa marehemu hakukimbizwa na gari la polisi bali yeye kutokana na kiwewe alichokuwa nacho gari ya polis ilismama barabarani kumzuia ambapo walikuwa wamefungua milanga ya gari ambapo walikuwa wakiendesha wamefungua milango jambo hilo lilimfanya dereva wa pikipiki kupata kiwewe nakujikuta akiangukia gari hilo nakupoteza maisha
Baada ya hapo tulizungumza na Baba mzazi wa marehemu huyo ilikujua kuhusian na kisa kilichomkuta mwanae ambapo amesema alipokea tarifa hizo kutoka kwa wasamalia kuwa mwanae amefariki baada ya kukimbizwa na gari ya polisi ambapo walikuwa wakimkimbiza alipokuwa amebeba samaki akiwa anawapeleka tarime kwa ajiri ya kuwauza na alipowaona polisi hao alianza kutetemeka nakupelekea kujigonga kwani walikuwa wamefungua milango ya gari hiyo ndipo akajigonga napikipiki yake nakufariki papo hapo.
Bwana hery amesema kwa kitendo alichofanyiwa motto wake sichakibindamu kwani nimmoja ya kuvunja sheria halua polisi anaeuhusiwa kumkibiza mwendesha pikipiki badala yake kutafta mbinu nyingine yakumkamata mtuhumiwa.
Alisema yuko tiari kufungua mashtaka aspopata maelezo yakutosha kutoka kwa kamanda wa polisi kanda maalum Tarime/Rorya.
Kwa upande wake kaimu kamanda akizungumza kwanjia ya simu na MAKALIBLOG alisema dereva pikipiki huyo ndio yeye aliyegonga gari hilo la polisi na siinavodaiwa kwamba polisi wamesababisha ajari hiyo.Alisema swetbert njewike kaimu kamanda wa jeshi lapolisi kanda maalum tarime Rorya.