VALENCIA AONGEZA MKATABA UNITED.
WINGA wa Manchester United, Antonio
Valencia amesaini nyongeza ya mwaka mmoja
katika mkataba wake ambao utamuweka
hapo mpaka mwaka 2019 huku kukiwa na kipengele cha kuongezewa tena.
Valencia mwenye umri wa miaka 31
amecheza mechi 43 za mashindano yote za United msimu huu na kukiongoza kikosi
cha timu hiyo kama nahodha wakati walipotwaa taji la Europa League mbele ya
Ajax Amsterdam juzi.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ecuador alijiunga
na United akitokea Wigan Athletic mwaka 2009. Akizungumza na wanahabari, Valencia
amesema amefurahia sana mkataba huo kwani klabu hiyo imekuwa sehemu ya maisha
yake toka alipojiunga nao mwaka 2009.
Na MAKALIBLOG.TOA MAONI YAKO NA TANGAZA NA MAKALIBLO.
MATUSI HAPANA