TASAF YASIKITISHWA NA WALENGWA KUTOTIMZA MASHARTI.
Mmoja wa wanufaika wa TASAF III katika Kijiji cha Migato akipokea fedha katika zoezi la uhawilishaji lililofanyika kijijini hapo jana.
Baadhi
ya wanufaika wa TASAF III wa Kijiji cha Migato wakiimba wimbo maalum wa
kuwakaribisha wataalam kutoka TASAF Makao Makuu, Benki ya Dunia na wadau
wengine wa maendeleo (wadau washiriki wa mradi) ambao ni UNDP, UNFPA, ILO na
Umoja wa Nchi za Ulaya(EU) waliofika kufanya tathmini ya utekelezaji wa mradi
wa TASAF III Wilayani Itilima mkoani Simiyu. (PICHA ZOTE NA COSTANTINE MATHIAS-SIMIYU).
MFUKO wa
Maendeleo ya Jamii (TASAF) umesikitishwa na kitendo cha wanufaika kutotimiza
masharti ya mpango huo hali inayosababisha kukosa fedha katika ruzuku hiyo kwa
kaya maskini.
Hayo
yalibainishwa jana na Mkurugenzi wa Ukaguzi wa ndani kutoka makao makuu (TASAF) Christopher Sanga alipotembelea
wanufaika katika kijiji cha Migato wilayani Itilima mkoani Simiyu na kusema
kuwa lengo la serikali kuwanufaisha ni kuwakwamua kimaisha.
Alisema kuwa
serikali inatoa fedha hizo kupitia ruzuku ya masharti ili watoto waweze kupata
mahitaji yao ya kila siku ikiwemo huduma ya elimu na matibabu kwa kupelekwa
kliniki.
Sanga
aliwataka wazazi kuwapa nafasi ya kwenda shule watoto ili kutimiza masharti ya
mpango huo ana pia wawze kufikia malengo ya serikali ya kunusuru familia zao.
‘’mnaonekana
kurudisha nyuma jitihada za serikali ambazo lngo lake ni kuwaondoa katika hali
mliyokuwa nayo awali ya umasikini na kupiga hatua kimaisha katika kukidhi
mahitajia ya kila siku’’ alisema Sanga.
Aliongeza
kuwa changamoto ya kutotimiza masharti kwa wanufaika hao bado ni tatizo hali
inayosababisha kaya kupoteza ruzuku yake na kupungua kwa malipo ya wanufaika.
Alisema kuwa
Lengo la serikali ni kujenga nguvukazi ya watu wake katika kutatua kero za wananchi
na mtoto asipopelekwa kliniki akiwa mdogo, uzalishaji utapungua akiwa mkubwa.
Nao baadhi
ya wanufaika wa mpango huo walikiri kuwepo kwa baadhi ya familia kutotimiza
masharti ya ruzuku hizo na kusababisha fedha kurudishwa TASAF makao makuu.
‘’kuna
baadhi ya familia watoto hawafiki shuleni, lakini asubuhi wanaaga na kuvaa sare
kwenda shule…hivyo ni jukumu la kila mzazi kuhakikisha mtoto wake anahudhuria
masomo ili aweze kutimiza masharti ya mpango huu’’ alisema Minza Bulayi Mkazi
wa Migato.
Katika
kipindi cha mwezi Novemba hadi Disemba kaya 29 kati ya 99 kijijini hapo
hazikuchukua ruzuku kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo walengwa kushindwa
kutimiza masharti ya Elimu na Afya kwa lengo la kuwa na jamii yenye afya na
elimu bora kwa watoto.


