MAN CITY YANASA KIUNGO WA MONACO.
KLABU ya Manchester City imekubali
kutoa kitita cha paundi milioni 43 kwa ajili ya kumsajili kiungo wa kushambulia
Bernardo Silva kutoka kwa mabingwa wa Ufaransa Monaco.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno
mwenye umri wa miaka 22, anatarajiwa kujiunga na City pindi dirisha la usajili
la majira ya kiangazi likapofunguliwa Julai mosi mwaka huu huku klabu
ikitarajiw akutangza usjaili huo Alhamisi ijayo.
Silva amecheza mechi 58 akiwa na
Monaco msimu huu zikiwemo mechi mbili dhidi ya City walizokutana katika
michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambapo amefunga mabao 11 na kusaidia
mengine 12. Nyota huyo pia ameichezea Ureno mara 12 na kufunga bao moja