Trump amfuta kazi mkurugenzi wa FBI James Comey

Rais Donald Trump
amemfuta kazi mkurugenzi wa shirika la ujasusi la FBI kutokana na hatua
yake ya kuliangazia swala la barua pepe za aliyekuwa mgombea wa uraisi
wa chama cha Democrat Hillary Clinton, mamlaka imesema.
Ikulu ya Whitehouse iliishangaza Washington kwa kutangaza kwamba James Comey amefipigwa kalamu.
Lakini wanachama wa Democrats wamesema kuwa alifutwa
kazi kwa sababu FBI ilikuwa ikuchunguza madai ya uhusiano kati ya Trump
na Urusi.
Hatua hiyo inajiri baada ya kubainika kwamba bwana
Comey alitoa habari za uongo kuhusu barua pepe za Clinton kwa bunge la
Congress wiki iliopita.
Rais Trump aliandika barua kwa bwana Comey kwamba alikubaliana
na mapendekezo ya mwanasheria mkuu Jeff Sessions kwamba ameshindwa
kuliongoza vizuri shirika hilo.
Bwana Sessions alisema kuwa idara ya haki ina nidhamu ya hali ya juu, uadilifu na sheria na mwanzo mpya unahitajika.
Ikulu ya Whitehouse imesema kuwa utafutaji wa mrithi wake unaanza mara moja.
Naye
kiongozi wa chama cha Democratic katika Bunge la Seneti, Bwana Chuck
Schumer, amesema kuwa ni wakati mwafaka sasa kumteua kiongozi maalumu wa
mashtaka kusimamia uchunguzi huo juu ya uhusiano na Urusi.
Alisema kuwa hatua hiyo isipochukuliwa raia wa Marekani wana
haki ya kuwaza kuwa Bwana Comey amefutwa ili kupunja juhudi za
kukamilisha uchunguzi huo.
Ikulu ya White House imekanusha kuwa kutimuliwa kazini kwa Bwana Comey kuna uhusiano wowote na maswala ya kisiasa.