Mkurugenzi wa kampuni ya ndege apigwa chapati ya uso Australia;

Hotuba ya mkurugenzi wa shirika la ndege la Australia Airline Qantas ilisitishwa kwa muda baada ya kupigwa na chapati usoni.
Alan
Joyce alikuwa akihutubia mkutano wa biashara katika eneo la Perth
wakati mtu mmoja alipopanda jukwaani na kumpiga chapati ya uso.
Mtu huyo alikamatwa na maafisa wa usalama .
Maafisa wa polisi wanasema kuwa wanamuhoji.
Bwana
Joyce alikuwa akizungumza kuhusu hatua ya safari ya moja kwa moja
kutoka London hadi Perth bila kusimama katika vituo vilivyopo.
''Sijui hilo lilisababishwa na nini '',aliwaambia takriban watu 500 waliokuwa wakisikiliza hotuba yake.
Bwana Joyce aliondoka katika jukwaa hilo kwa muda ili kusafisha uso wake kabla ya kurudi akishangiliwa.
''Sasa iwapo kuna chapati nyengine tafadhali malizeni shughuli yake'', alisema.
sourec bbc.