TADB, SUA WAINGIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB),
Bw. Francis Assenga (katikati) akiongoza kikao cha majadiliano juu ya
ushirikiano na Chuo cha Kilimo cha Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) wakati
uongozi wa Chuo hicho walipotembelea Ofisi za TADB. Msafara wa huo wa
Chuo cha Kilimo uliongozwa na Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Susan
Nchimbi-Msolla (wapili kulia) na msaidizi wake Prof. Benard Chove
(kulia). Wengine pichani ni wajumbe wa menejimenti ya TADB.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB),
Bw. Francis Assenga (wapili kushoto) akibadilishana hati za makubaliano
na Mkuu wa Chuo cha Kilimo cha Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA), Prof. Susan
Nchimbi-Msolla. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Sheria na Huduma wa TADB, Bibi
Neema-Christina John (Kushotot) na Naibu Mkuu wa Chuo cha Kilimo cha
Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA), Prof. Benard Chove (kulia). Makubaliano
hayo yalisainiwa katika Ofisi za TADB, Dar es Salaam.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB),
Bw. Francis Assenga (wapili kushoto) and Mkuu wa Chuo cha Kilimo cha
Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA), Prof. Susan Nchimbi-Msolla wakionesha hati
za makubaliano. Makubaliano hayo yanalenga uendelezaji wa masuala ya
utafiti na kujengea uwezo wa kitaasisi baina ya pande hizo mbili.
Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Sheria na Huduma wa TADB, Bibi Neema-Christina
John (Kushoto) na Naibu Mkuu wa Chuo cha Kilimo cha Chuo Kikuu cha
Kilimo (SUA), Prof. Benard Chove (kulia).