ANGALIA MATUKIO YA MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA MASHAURIANO WA BODI WA MAKANDARASI MJINI DODOMA
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame
Mbarawa muda mfupi kabla ya kufungua mkutano wa Mashauriano Wa Bodi ya
Usajili wa Makandarasi kwa Mwaka 2017 kwenye ukumbi wa Kimataifa wa
Mikutano wa Kikwete mkoani Dodoma.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano Wa Bodi ya
Usajili wa Makandarasi kwa Mwaka 2017 kwenye ukumbi wa Kimataifa wa
Mikutano wa Kikwete mkoani Dodoma.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa,Viongozi wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi na Wajumbe waliohudhuria mkutano wa Mashauriano Wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi kwa Mwaka 2017 nje ya ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kikwete mkoani Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa,Viongozi wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi na Wajumbe waliohudhuria mkutano wa Mashauriano Wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi kwa Mwaka 2017 nje ya ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kikwete mkoani Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
…………….
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
ameagiza kuwa miradi yote yenye thamani isiyozidi bilioni 10 wapewe
Wakandarasi wa ndani hasa kwa miradi inayotekelezwa kwa fedha za ndani
kwani wakandarasi hao watasaidia kuongeza ajira kwa vijana wa Kitanzania
na kuongeza uwekezaji ndani ya nchi.
Makamu
wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo mjini DODOMA wakati
anafungua mkutano wa siku Mbili wa mashauriano wa Bodi ya Usajili wa
Wakandarasi mwa mwaka 2017.
Makamu
wa Rais amesisitiza wakandarasi hao kufanya kazi zao kwa kuzingatia
maadili na sheria pamoja na kumaliza kazi wanazopewa ndani ya muda
uliopangwa kwa kuzingatia ubora wa kazi na gharama zilizokubalika kwenye
mikataba na sio vinginenevyo.
Makamu
wa Rais amewataka wakandarasi kote nchini kuacha mara moja tabia ya
kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa ili kuongeza ufanisi katika
utekelezaji wa miradi ya ujenzi wanayopewa.
Amesema
kuwa Serikali itaendelea kuwapa kipaumbele wakandarasi wazawa ili
wathubuti kujitosa na kumudu zabuni za ujenzi kwani kwa kufanya hivyo
kutaleta faida mbalimbali ikiwemo fedha watakazopata watawekeza ndani ya
nchi na kutoa ajira za kutosha kwa vijana wa Kitanzania.
“Hatuwezi
kuwa na Tanzania ya Viwanda huku tukiwanufaisha Makandarasi wa nje
pekee ni lazima Makandarasi wa ndani wanufaike pia.”
Kuhusu
madeni ya wakandarasi, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan
amewahakikishia wakandarasi kuwa Serikali haijawasahau na bajeti ya
Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano ambayo imepitishwa na bunge
imezingatia kilio hicho cha wakandarasi.
Ameahidi kuwa Serikali itaendelea kulipa madeni inayodaiwa na wakandarasi ili kujenga mahusiano mazuri ya wakandarasi hao.
Kwa
upande wake, Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa amesisitiza kuwa Wizara hiyo inaendelea kusimamia sheria na
maadili kwa wakandarasi ili kuhakikisha miradi ya ujenzi inayotekelezwa
kote inakuwa na ubora unaotakiwa.
Waziri
Profesa Mbarawa amekiri kuwa kuna baadhi ya wakandasiri ambao
hawatekelezi majukumu yao ipasavyo hivyo kujenga miradi jinsi ya kiwango
hivyo ni muhimu kwa wakandarasi hao kufanya kazi kwa ubora ili waweze
kuaminiwa na Serikali na kupewa kazi.
Amesema
kuwa Wizara yake itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuwajengea uwezo
wakandarasi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa viwango
vinavyotakiwa.
Nae,
Msajili wa Bodi ya Wakandarasi Nchini Rhoben Nkori amesema bodi hiyo
imefuta usajili wa wakandarasi 3,000 kwa kushindwa kutimiza matakwa ya
Usajili wa Wakandarasi ya mwaka 1997 na kwa sasa bodi hiyo
inawakandarasi 9,000 kote nchini.
Msajili
huyo pia amesema kuwa katika kuratibu mwenendo wa kazi za makandarasi
bodi hiyo ilikagua miradi 3,813 ambapo kati ya miradi hiyo miradi 2714
sawa na asilimia 71.2 haikuwa na kasoro na miradi mingine ilikuwa na
kasoro mbalimbali ikiwemo miradi hiyo kutofanywa na wakandarasi
waliosajiliwa na kutozingatia usalama wa wafanyakazi.
Kasoro nyingine ni wakandarasi kufanya kazi zaidi ya viwango vya madaraja yao,miradi kutosajiliwa na miradi kutokuwa na bango