RT YAMPONGEZA MSHINDI MBIO ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI.


Displaying P1030528.JPG

Rais wa Riadha nchini Anthony Mtaka akimpongeza mshindi Frank Kwilasa wa mbio za mita 400 za Mashariki na kati zilizofanyika jijini Dar-es-Salaam kwa kusishirikisha nchi 11.Na COSTANTINE MATHIAS, Maswa-Simiyu.
CHAMA cha Riadha nchini Tanzania kimempongeza mshindi wa mbio za mita 400 za Afrika Mashariki na Kati zilizofanyika jijini Dar-es-Salaam kwa baada ya kujinyakulia medali ya dhahabu.

Pongezi hizo zilitolewa na Rais wa Chama hicho Anthony Mtaka
ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Simiyu ambapo mshindi wa mbio hizo anatokea wilayani Maswa mkoani Simiyu
.

Mtaka alimtaja mshindi huyo kuwa ni Frank Onesmo Kwilasa aliyeshika nafasi ya kwanza katika mbio hizo na kujinyakulia medali ya dhahabu huku akiwa ni mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule kutwa ya Sekondari mwasayi wilayani Maswa.

Rais huyo aliwataka vijana wengi kujitokeza katika kushiriki mbio mbalimbali za riadha kwa kuonysha uthubutu huku akiahidi kuonyesha ushirikiano kwa vijana watakaojitokeza kushiriki riadha.

Katika hatua nyingine Mtaka amemhamisha mwanafunzi huyo na Mwalimu wake wa michezo toka shule ya kutwa Mwasayi kwenda shule ya Bweni ya Binza iliyoko mjini Maswa ili aweze kuendelza kipaji chake.

Awali kwa upande wake Frank Onesmo alisema kuwa yeye anatoka familia maskini na amekuwa akiishi maisha magumu lakini amekuwa akijituma katika michezo na kusikiliza ushauri wa mwalimu wake wa michezo.

‘’natokea familia duni, nimepanga chumba ili kusogea shuleni…mazoezi na kujituma ndiyo siri ya mafanikio haya nina ndoto za kuwa mkimbiaji wa kimataifa, niwaombe vijana wajitahidi kwa sababu mtu hawezi kukutambua bila wewe kujitambua’’ alisema Frank.

Kwa upande wake mwalimu wa Michezo wa mchezaji huyo Gladius Rwezaula alisema kuwa anampongeza Rais wa Riadha kwa kumsaidia kijana huyo kumhamishia shule ya bweni ili aweze kutimiza ndoto zake.

Rwezaula aliongeza kuwa changamoto zinazowakabili wanamichezo mkoani Simiyu ni ukosefu wa viwanja vyenye vipimo sahihi na kuitaka serikali na shirikisho la Riadha nchini kuweza kutatua changamoto hiyo.

Mashindano hayo ya mita 400 yalifanyika jijini Dar-es-Salaam ambapo yalishirikisha nchi 11, mshindi wa kwanza alijinyakulia medali ya dhahabu, mshindi wa pili medali ya fedha na mshindi wa tatu medali ya shaba.
 Displaying P1030525.JPG
Powered by Blogger.