Meneja SIDO Mkoa wa Mara Frida Mungulu akiongelea fursa zilizopo katika Mkoa wa Mara katika Mkutano huo.
Meneja wa Sido mkoani Mara Bi.Frida Mungulu amewataka wandishi wahabari mkoani humo kuzitumia kalamu zao kuzitangaza fursa zilizopo mkoani kwani ndio chachu ya kauli mbiu ya kumuunga mkono Raisi wa jamhuri ya muungano wa tanzania katika sera yake ya Viwanda.
Aliyasema hayo katika Maadhimisho ya Siku ya uhuru wa vyombo vyahabari ambapo siku hiyo huadhimishwa kila ifika may tatu na chama cha wandishi wa habari mkoani humo kimefanya maadhimisho hayo may kumi na tisa.
kauli mbiu katika maadhimisho hayo ''Sasa ni wakati wa Habari za Uwekezaji katika Viwanda Mara'' ambapo ndipo Bi.Frida akatumia nafasi hiyo kama mdau kwasihi wanahabari wa mara kutangaza kwani zipo fursa nyingi sana ambazo zinafanyika katika mkoa huo nazinahitajika kuiburiwa na wengine wazifahamu.
Tukitolea mfano wilaya ya tarime kuna ndizi nyingi ambazo zinaweza kutangazwa naikapatikana elimu ikatolewa angalau hata unga wandii kazi yake nini wafundisheni watu waelewe.alisema Bi, Frida Mungulu.
Pia alisema kwa kushirikia na Wanahabari na watumishi wa serikali kuunganisha nguvu ya pamoja upo uwezekano mkubwa wakuzitangaza Fursa zilizopo mkoani mara.
Nami natumia nafas hii kama mmiliki wa MAKALIBLOG.nawaomba wandishi wezangu mlioko mkoani mara nahata mlionje ya mkoa huu tumieni kalamu zenu kutoa na kuibua viwanda na na fursa zilizoko mikoani mwenu nahata pia kuibua viwanda vidogo vidogo ambavyo havifahamiki kwa kutumia kalamu zenu hii inaweza kuwa nimmoja ya jitiahada ya kumuunga mkono Rais wa Nchi hii katika Safari ya Viwanda.
Aidha kupitia kwa meneja wa Sido Mkoani Mara Bi.frida kwa kushirikiana na uongozi wako tumieni nafasi kama hizi kukutana na wandishi wa habari ilikuwapa mafunzo kuhusiana na kile ambacho mnakifanya katika maeneo yenu ikiwamo kuwapa mafunzo wanahabri yatayo wajenga zaidi wakati wakuandika nahata na wao ambao ni mabarozi wazuri wakupeleka Elimu hii katika jamii zinazo wazunguka.
Namaliza kwa kusema sote kwa ummoja na kwakushirikiana tutafanikiwa kuifikisha safari hiii panapotakiwa kwa umoja na nguvu na ushirikiano wetu pamoja.
Waandishi wa Habari pamoja na Wadau wa Habari katika Mkutano huo.
Mwenyekiti wa TCCIA Bonephace Ndengo akiongea na wadau wa Habari.
Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa klabu ya Wandishi wa Habari Mkoa wa Mara Mugin Jacob Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt Charles Mlingwa akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Musoma Mjini Vicent Naahano katika Mkutano huo wakimfatiria meneja wa SIDO.
HONGERA BI.FRIDA KWA ELIMU YAKO UNAYOITOA KWA WATANZANIA KUHUSIANA NA KUELEWA KUHUSU VIWANDA.