MKUU WA MKOA WA MARA AWATAKA WAWEKEZAJI KUFUFUA VIWANDA VYA SAMAKI MKOANI HUMO; UNAWEZA KUTIAMA PICHA ZA MATUKIO YOTE YA KIKAO HICHO;

 Alie simama ni mkuu wa mkoa wa mara dkt Charles Mlingwa kushoto kwake ni mkuu wa wilaya ya musoma DK Vicent Naahano kulia kwake ni meya wamanispaa ya musoma Mheshimiwa GUMBO.
Na MAKALIBLOG.MUSOMA, MARA
Mkuu wa mkoa wa mara dk charles mlingwa amewata wawekeaji kuanza kufufua viwanda vya samaki vilivyokuwa vimefungwa maana samaki wapo wakutosha.
MPANGO  mkakati  wa utunzaji wa mazingira katika ziwa Victoria umezinduliwa  katika nchi tatu za Uganda , Kenya na Tanzania ili kutunza rasilimali zilizomo na kuweza  kukuza uchumi  wa wananchi .

 mpango huo umezinduliwa jana naMkuu  wa Mkoa wa Mara  Dk. Charles Mlingwa  katika ukumbi wa Uwekezaji uliopo ofisi ya mkuu wa mkoa.

Dk. Mlingwa alisema  nchi tatu hizo hazina budi  kufanya ulinzi shirikishi  katika  utunzaji wa mazingira  wa ziwa victoria  ambao nikama mgodi wa asali ambao utakuza uchumi  ifikapo 2020 tuweze kuondokana  na umaskini.

‘’Panahitajika  ulinzi shirikishi kwa nchi hizi tatu ili ziwa hili lisitumiwe  na maharamia na kutumiwa kupitisha magendo’’alisisitiza.

Aidha aliongeza kuwa endapo  watatimiza wajibu wao  katikakutekeleza majukumu ya kazi zao wataweza kufanya matumizi endelevu ya rasilimali zilizomo ndani ya  Ziwa hilo.

Amewataka pia kuungana kwa pamoja na kuhakikisha  wanapiga vita uvuvi haramu  kwa kuzuia nyenzo haramu na kuwadhibiti  wanaotumia sumu katika uvuvi haramu bali watumie ziwa hilo ipasavyo  katika kuinua  uchumi  wa Afrika Mashariki kwa kuwekeza  katika viwanda vya samaki na kuibua miradi mbalimbali itokanayo na ziwa hilo.

Amewashauri pia kutumia  vizuri ziwa hilo  katika kilimo cha umwagiliaji kwa kuangalia mabadiliko ya tabia ya nchi  na kuwawezesha wananchi wapate miundombinu ya kilimo endelevu ili  waweze kuepukana na njaa .

Naye Kaimu  katibu  Mkuu Ushirikiano wa halmashauri zinazozunguka ziwa Victoria  Edwin Magere alisema nia ya uzinduzi huo wa mpango mkakati  wa utunzaji  mazingira wa ziwa victoria  kwa njia nyingine ni kuwashirikisha wadau wote wa chini ili kuboresha utunzaji wa mazingira katika ziwa hilo.


Kwa upade wake mkuu wa wialaya ya Musoma DAKTAR VICENT NAANO. ambae pia amekuwa akishiriki kwa ukubwa na ulinzi wa ziwa victoria hasa kupamabana na uvuvi haramu amesema ipo haja ya kuweka sheria ndogo ndogo kwa ajiri ya ya kulinda ziwa hilo.

amesema bila kuweka sheria hizo itakuwa nikama wanancheza tu tarabu  lakini kama itakuwepo jitihada na sheria kali itafanya kuliweka ziwa vizuri nakupata samaki ambao wakao tiari kwa ajiri ya matumizi.




 Wajumbe wa mkutano wakujadiri mazingira kutoka nchi tatu TANZANIA, KENYA ,NA UGANDA.


 Wajumbe wakifatiria kilichokuwa kinawsilishwa katika kikao hicho.



 DKT Vicent Naahano akizungumzia mkuhusia na utunzwaji wa ziwa victoria ambapo amekuwa nimmoja ya viongozi waliopambana na uvuvi haramu.


 wajumbe kutoka maeneo mabalimbali wakisikiliza mkuu wa mkoa wakati akizindua  mpango kazi huo.



                                               TANGAZA NA MAKALIBLOG
Powered by Blogger.