MARA-RC WAHISI UJANJA UJANJA BODI YA PAMBA WASHINDWA KUTEKELEZA MAAGIZO YA MKUTANO MKUU;

 
Na Mwadishi wetu Costantine Mathia;
MAKALIBLOG; SIMIYU;
 Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe.Dkt.Rehema Nchimbi (wa pili kushoto) akichangia jambo wakati wa ziara ya wakuu wa mikoa ya Kanda ya Magharibi inayolima pamba  walipotembelea mashamba ya uzalishaji wa mbegu bora ya pamba(UKM08) katika kata ya Mwabusalu wilayani Meatu(kulia) Mkuu wa Wilaya ya Bariadi,Mhe.Festo Kiswaga ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka.
Wakati lawama kubwa za wakulima wa pamba zikiwa ni kuuziwa mbegu zisizoota na dawa zisizokuwa na ubora, wakuu wa mikoa inayolima zao hilo wasema bodi ya pamba Tanzania (TCB) inaendeshwa kiujanja ujanja.

 Wakuu hao wa mikoa inayolima zao la pamba nchini wamesema kuwa bodi ya pamba wameshindwa kutekeleza maagizo ya mkutano mkuu wa wadau wa kuwa na mashamba ambayo yatakuwa yakitumika kwa ajili ya kuzalisha mbegu za zao hilo.

Hayo yalibainishwa juzi na wakuu wa mikoa hiyo yaShinyanga,Geita,Singida,Kigoma ,Tabora na Simiyu wakati wa ziara ya kutembelea shamba la mfano lililopo katika kijiji cha Mwabusalu Wilayani Meatu walipokwenda kujifunza jinsi ya kulima zao hilo ikiwemo mbegu ya Ukm 08.


Akiongea kwenye Shamba hilo Mkuu wa mkoa wa Geita Meja Jenerali mtaafu Ezekiel Kiunga alisema kuwa bodi ya pamba wamekuwa wajanjawajanja na wameshindwa kutekeleza maagizo waliyopewa ya kuwa na mashamba yao wenyewe ya kuzalisha mbegu na badala yake wanatumia mashamba ya wananchi.


“Bodi ya pamba inaendeshwa kihuni kila wakipewa maelekezo wanashindwa kutekeleza kutekeza mwaka jana katika mkutano mkuu tuliwataka kuanzisha mashamba yao ya kuzalisha mbengu ya pamba ili kuondokana na kutegemea kutoka kwa wananchi lakini bado wanategemea wananchi kuzalisha”alisema Kiunga.


Alibainisha kuwa wanakuwa na wasiwasi na utendaji kazi wa bodi ya pamba kwani yale wanayokubaliana kwenye vikao yanabaki kwenye makaratasi na kushindwa kufanyiwa kazi na kubaki kuwaumiza wananchi wanaolima zao hilo.


Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Tabora Agrey Mwanri  alisema kuwa kilimo cha pamba kitakufa  endapo wananchi hawatawezeshwa  kuingia katika kilimo cha mkataba ambacho ataingia na mnunuzi moja kwa moja kwani itawawezdesha kupata mahitaji yote ya pembjeo.


“njia pekee ya kumsaidia mwananchi anaylima zao hili ni kumuweka katika kilimo cha mkataba kwani ataweza kupata pembejeo kwa bei nafuu kulimo kumwacha anajigharamia mwnyewe kwani inafika mahali mkulima huyu anakosa hela ya kuhudumia”alisema Mwanri.


Naye Mkuu wa mkoa wa Singida Dk Rehema Nchimbi alisema ni bora bodi iwe inafanya tafiti katika maeneo mbalimbali ya mbegu za pamba kwani eneo la simiyu halifanani na eneo la mkoa wa singida hivyo mbegu zinazostawi simiyu singida haziwezi kustawi ni bora ikaangaliwa njia nyingine za kuzifanyia mazoezi.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya kuchambua pamba la Gaki  kutoka shinyanga Gasper Kileo alisema kuwa njia peke ya kuweza kuingia katika kilimo cha mkataba ni kuazisha ushirika na kufufua iliyokuwa mifuko ya ushirika ambao watakuwa wanasimamiwa na serikali wataweza kufanya kazi vizuri na wakulima.


Alibainisha kuwa lazima ushirika wafanye uchaguzi na usimamiwe na serikali kwani tukiwaacha wenyewe hawataweza kupata viongozi ambao wataweza kuwasaidia wananchi na kutatua changamoto zao.



 Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba, Marco Mtunga akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali kwa wakuu wa mikoa ya Kanda ya Magharibi inayolima pamba  walipotembelea mashamba ya uzalishaji wa mbegu bora ya pamba(UKM08) katika kata ya Mwabusalu wilayani Meatu
 Baadhi ya Wakuu wa mkoa ya Kanda ya Magharibi inayolima pamba  wakati wa ziara yao walipotembelea mashamba ya uzalishaji wa mbegu bora ya pamba(UKM08) ya katika kata ya Mwabusalu wilayani Meatu.




KWA USHAURI UNAWEZA KUTUPIGIA KUPITIA 0754295996,0789524987 ‘’’ MATUSI HAPANA
 


Powered by Blogger.