MGANGA HOSPITALI, MBARONI KWA KUOMBA RUSHWA YA SHILINGI Tshs.20000 KWA MJAMZITO;

Na.MAKALIBLOG.MARA.
Tasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Mkoani
mara imemfikisha mahakamani mganga wa hospitali ya wilaya Tarime Samweli Isaya
obierokwa kosa la kudai na kupokea rushwa kiasi cha shilingi elf ishirini
20000/= ,
kutoka kwa magesa kihongo ili aweze kumhudumia mkewe aliekuwa mjamzito.
Obiero akiwa mwajiriwa wa halmashauri ya tarime
katika hospitali hiyo alipokea kiasi hicho cha fedha kutoka kwa mwananchi ambae
alifika na mkewe kwa ajiri ya kupata matibabu kutokana na na tatizo la ujauzito
lilokuwa likimkabili.
Kwa kutambua kuwa hilo nikosa kisheria lakini
tabibu huyo anadaiwa kuomba kiasi hicho cha fedha ilihali yeye akiwa ni
mtumishi wa umma anaestahili kutoa huduma hiyo,
Wakati huo huo tasisi hiyo pia imempandisha
kizimbani mkuu wa soko la Bweri Maanya manyama kwa kosa la kupokea rushwa kiasi
cha shilingi elf kumi nambili kutoka kwa mtu mmoja ambae jina lake
limehifadhiwa baada ya kukutwa akijisaidia katika maeneo yasiyo ruhusiwa ndani
ya soko hilo.
Ambapo inadaiwa kuwa maanya akiwa mkuu wa soko
hilo akishirikiana na askari mgambo Wiliam mafuru walipokea kiasi hicho cha
pesa ili wasimchukulie hatua za kisheria mwananchi aliekutwa akijisaidia katika
eneo hilo lisilo ruhusiwa.
Kwa kutambua kuwa kitendo cha kupokea rushwa
nikinyume cha sheria kifungo cha 15(1) (a) yakuzuia na kupambana na rushwa ya mwaka 11/2017.
maanya
manayama alikana mashitaka yake na
kutakiwa kuwa na wadhamini wawili kwa dhamana ya maandishi ya million nne kila
mmoja hivyo akashindwa kutimiza masharti hayo na kupelekwa mahabusu.
Mahakama imetoa hati ya kupelekwa kwa washitakiwa
Wiliam Mafuru na Victor Chrisma,ambapo
washitakiwa hao wawili wapo mahabusu katika kesi nyingine namba CC37/2017.
Aidha kesi hiyo ya rushwa namba CC 299/2017
imefikishwa mahakamani hapo na mwendesha mashitaka wa TAKUKURU Mwinyi
yahaya na iko mbele ya Hakimu wa
mahakama hiyo Mheshimiwa Amon Kahimba.