MKUU WA MKOA WA MARA AKAGUA MIRADI YA UJENZI WA BARABARA MKOANI HUMO,ATOA ONYO KALI KWA WAFUGAJI

 Image result for MLINGWA

Image result for MLINGWAMkuu wa mkoa wa mara DK.Charles Mlingwa amepiga marufuku ufugaji wa mifugo katikati ya miji ya mkoa wa mara ambapo imekuwa ni mmoja ya uharibifu wa miundombinu zikiwemo barabara.

Ameyasema hayo wakati akihitimisha ziara ya ukaguzi wa miradi ya kitaifa ya ujenzi wa barabara mkoani mara alisema kuwa kuanzia sasa nikosa kufuga mifugo katikati ya mji na ataandika barua kuwaelekeza wakuu wawilaya zote za mkoa huo ikiwemo kubomoa mabanda yote ya mifugo yaliyoko katikatiya wilaya za mkoa huo.
DK.Charles Mlingwa amefayaziara ya kukagua miradi ya kitaifa ya ujezi  na ukarabati wa barabara  za mkoa wa Mara ambapo amewataka wakandarasi kukamilisha miradi waliyopewa kwani ndio tegemeo kwa wananchi wamkoa huo ambapo itarahisisha usafirishaji wa biashara zao mazao pamoja na utalii.
Miradi ya ujenzi na ukarabati wa barabara inayokamilishwa mkoani mara nipamoja na barabara ya simiyu na mara mpakani musoma yenye km 85.5ambapo barabara hiyo ikiwa kipindi  chamatazamio zilijitokeza kasoro eneo la suguti na baada ya kufahamika kasoro hizo mkandarasi aliagizwa kulekebisha.

 Katika ujenzi wa kiwango cha lami wa barabara ya makutano juu-Natta,Mugumu,liondo na Mto wambu sehemu ya Makutano Juu Sanzate wenye km50 ambapo ujenzi huo unaendelea mkuu wa mkoa wa mara amemuagiza mkandarasi kuharakisha kukamilisha ujenzi wa babarabara zalami ambapo Utalii wa mara ni mgodi wa biashara juu ya ardhi.

DK.mlingwa ameigaiza ofisi ya meneja wa tanirods mkoa wa mara kuwaita wakandarasi wazalendo wote ilikuwa fahamisha jinsi serikali inavyofanya kazi zake baada ya kutoridhishwa na kasi ya ujenzi na ukarabati wa lami nyepesi   wa barabara ya mika,utegi hadi shirati.


Pia meneja wa tanroads mkoani mara Enginia Mlima Felix ngaila amewataka wananchi kutokujenga kando ya barabara ilibadae walipwe yaani tegesha ambapo watakuwa wanajidanganya nakupoteza mda wao bure kwambawatapata fidia ambayo yeye ameichukulia kama changamotokatika ziara hiyo.
Aidha mkuu wa mkoa wa mara ametembelea miradi ya ujenzi na ukarabati wa barabara ikiwemo wilaya za Bunda,butima,serengeti,tarime,rorya pamoja na musoma ambapo pamoja nakuwataka wakandarasi kuharakisha kukamilisha miradi hiyo lakini pia zimekuwa zikikumbwa  na changamoto mbalimbali ikiwemo kugusa wananchi ,miundo mbinu mbalimbali ikiwemo nguzo za umeme nk,ambapo jumla ya km 1,273.09 huku hangarawe zikiwa 206.75 changarawe 1,066.34
Powered by Blogger.