Kauli ya Jerry Muro baada ya Haji Manara wa Simba kufungiwa na TFF
Muda
mfupi baada ya shirikisho la soka Tanzania TFF kupitia kamati ya
nidhamu ya TFF kutangaza kumfungia mkuu wa idara ya habari na
mawasiliano wa Simba Haji Manara kwa utovu wa nidhamu na kukutwa na
makosa matatu.
Afisa habari wa zamani wa Yanga ambaye nae alifungiwa mwaka mmoja Jerry Muro ametumia ukurasa wake wa instagram kuandika “Mtuache
sasa tupumzike, tuliyofanya kwa taifa hilo haswa kwenye mpira nadhani
yametosha, Waswahiba karibu kijiweni @hajismanara“
Mkuu
wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba Haji Manara amefungiwa mwaka
mmoja kujihusisha na soka pamoja na faini ya Tsh Milioni 9.
Kamati
ya nidhamu ya TFF imetoa adhabu hiyo licha ya Haji Manara kushindwa
kufika kwa madai ya kupata dharura lakini anayo nafasi ya kukata rufaa.