TFF WABADIRISHIA JUU GIA YA SIMBA POINTI 3 ZA KAGERA ZA REJEA;
Hatimaye
Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) imeipokonya pointi tatu Simba SC, ilizokuwa
imepewa kutoka kwa Klabu ya Kagera Sugar.
Awali,
Simba ilikuwa imepewa ushindi wa mezani wa pointi tatu na magoli matatu
dhidi ya Kagera Sugar, baada ya mchezo wake na timu hiyo ya mkoani
Kagera kumalizika ikiwa imepigwa magoli 2-1.
Ushindi
huo wa mezani ulitokana na malalamiko kuwa Kagera Sugar ilimchezesha
mchezaji aliyekuwa na kadi tatu za njano, hivyo hakuwa na sifa za
kushiriki mchezo huo kwa mujibu wa kanuni na sheria za Soka.
Akitangaza
uamuzi wa kurejesha matokeo ya awali ya uwanjani leo katika ukumbi wa
Habari wa TFF, Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Selestin Mwesigwa alisema
kuwa sababu zilizopelekea Kamati kuchukua uamuzi huo, ni pamoja na
kucheleweshwa kwa malalamiko ya Simba SC dhidi ya Kagera Sugar, Simba
kushindwa kulipia ada ya rufaa dhidi ya maamuzi ya mechi hiyo na
kukosekana kwa uhalali wa Kamati ya Saa 72 kwa kuwahusisha wajumbe
waalikwa ambao hawakuwa na sifa za kuwa kwenye kamati hiyo.
Kutokana
na uamuzi huo, Simba imeendelea kuwa kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania
Bara (VPL), ikiwa na pointi 59 badala ya 62 za awali.
Hali
hiyo inawapa nafuu ya kupumua watani wao wa jadi, Young Africans ambao
wana pointi 56 huku wakiwa na michezo miwili nyuma ya Simba FC.