Utafiti: Ndovu ndio mnyama anayelala kwa muda mfupi zaidi duniani
Wanasayansi waliowafuatilia ndovu
wawili nchini Botswana wamebaini kuwa wanyama hao hulala muda mfupi
zaidi ya mnyama mwengine yeyote duniani.
Ndovu hulala kwa saa mbili pekee hususan nyakati za usiku.
Wakiwa katika hifadhi, ndovu hulala kati ya masaa manne hadi sita kwa siku.
Ndovu hao wote wakiwa viongozi wa familia zao mara nyengine husalia macho kwa siku kadhaa na huonekana wakifunga macho ama kuota mara moja kila siku tatu ama hata nne.
Haijulikani kwa nini wanyama hao walio na uwezo mkubwa wa kukumbuka vitu wanaweza kuishi kwa kulala kwa muda mfupi licha ya usingizi kuwa na muhimu mkubwa katika ubongo .
nikwamuji ya bbcswahili.