Afya ya rais Robert Mugabe yadhoofika

 Zimbabwe
Rais wa Zimbambwe Robert Mugabe ameenda Singapore kufanya vipimo vya Afya yake, siku chache baada ya sherehe ya kufikisha miaka 93.

Mugabe amekua dhaifu zaidi, na sasa anapata shida hata kutembea wakati wa matukio mbalimbali ya kitaifa.
Msemaji wa rais huyo alisema kuwa vipimo hivyo ni vya mara kwa mara na Rais anatarajiwa kurejea nchini Zimbabwe wiki ijayo.
Mugabe ni kiongozi mwenye umri mkubwa zaidi duniani, aliingia madarakani mnamo mwaka 1980.
Powered by Blogger.