UKIMWI WA PUNGUA TANZANIA,,
NA; MAKALIBLOG; MUSOMA
IMEELEZWA
kiwango cha maambukizo ya VVU nchini kimepungua kutoka asilimia 7 mwaka 2003
mpaka asilimia 5.1 mwaka 2017 hali inayopelekea Tanzania kuwa miongoni mwa nchi
zilizo na kiwango cha chini cha maambukizo ya kati ya nchi za kusini mwa jangwa
la sahara.
Taarifa hiyo
iliyoandaliwa na wadau wa utafiti wa viashiria na matokeo ya ugonjwa wa UKIMWI
nchini ambapo ilisomwa na mkuu wa mkoa wa Mara Charles Mlingwa hivi karibuni wakati akifanya uzinduzi wa
utafiti huo mkoani hapa, kwamba mkutano huo uliwahusisha wadau hao wa sekta ya
afya uliofanyika katika ukumbi wa uwekezaji ofisi ya mkoa huo.
‘’Utafiti wa
aina hii ni wa nne kufanyika hapa nchini unaoangalia masuala ya afya ambapo
utafiti wa kwanza ulifanyika mwaka 2003/2004,wa pili ulifanyika mwaka 2007/2008
na utafiti wa tatu ulifanyika mwaka 2011/2012 ambapo tafiti hizi zilikuwa
zikihusisha wananchi wenye umri wa miaka 15 na 19’’alisema.
Alisema
utafiti wa mwaka 2016/2017 ni wa kipekee kwani kwa mara ya kwanza unahusisha
wananchi wa rika zote katika kaya zilizo chaguliwa sambamba na hilo utakuwa ni
utafiti wa kwanza kukusanya taarifa zinazohusiana maambukizo ya VVU kiwango cha
vvu mwilini kwa wanaoishi na vvu wastani wa maambukizo ya vvu kwa watu wa rika
zote na wingi wa chembechembe za kinga mwilini(CD4 T-Cell count)
‘’Utafiti
huu utaangalia pia kuwepo kwa viashiria vya usugu wa dawa,kiwango cha
maambukizo ya kaswende na homa ya ini(Hepatitis B na C) kwa watu wenye umri wa
miaka 15 na Zaidi,pamoja na hayo,utafiti huu utakusanya taarifa za upatikanaji
na utumiaji wa huduma zilitolewazo katika kudhibiti maambukizo ya vvu na UKIMWI’’alisema
Mlingwa.
Rc Mlingwa
alisema takwimu ya mwaka 2012 zinaonyesha robo ya wasichana nchini wenye umri
wa mwaka 14 na 17 walikuwa wamejifungua angalau mara moja lakini mikoa
inayoongoza kwa tatizo hili imetajwa kuwa ni Katavi asilimia 27.6 na Rukwa
asilimia 24.5 na kwamba tatizo hili pia lipo mkoani hapa linastahili
kushughulikiwa.
Aidha alisma
takwimu hizi zitasaidia kuboresha juhudi kubwa zinazofanywa na serikali za
kusogeza huduma zinazohusiana na vvu kama vile huduma ya upimaji wa virusi vya
ukimwi bure kwenye vituo vya kutolea huduma ya afya vya serikali
Huduma ya
kupunguza maambukizo ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT)
na utoaji wa dawa za kupunguza makali ya virusi hivyo zinazojulikana kama ARV.
Kutokana na
taarifa hiyo mkuu huyo wa mkoa huo aliwataka wananchi kuwapokea watafiti punde
tu watakapofika maeneo yao na kutoa ushirikiano wa karibu kwa wadadisi hao ili
kufanikisha zoezi hilo muhimu kwa taifa letu.
Kwa upande
wake afisa mawasiliano na uhamasishaji jamii Mihayo Bupamba alisema utafiti utafanywa
na wauguzi wote nchini waliochaguliwa kwa sheria ambapo watatumia teknolojia
kwa kudodosa na kompyuta,ipadi chombo kidogo chepesi kinachomrahisishia
mkusanyaji kupata taarifa.
‘’Mkoa wa Mara
sampuli imechaguliwa maeneo 12 ambayo ni wilaya ya Tarime kijiji cha Mangucha,Tarime dc Kata Nyamaranga kijiji
Gitagasembe,wilaya Serengeti kata Ring’wani
kijiji Nyamitita,Musoma dc kata Mugango kijiji Kwibara, Bunda dc Kata Igundu
kijiji Igundu, Rorya kata Nyahongo kijiji Ryagati, Rabour Oliyo,Butiama kata
Buswahili kijiji Wegero,Butiama dc Nyegina kijiji Mkirira, Bunda mjini Kata Kabarimu Musoma manispaa Kamunyonge
uwanja wa ndenge’’alisema.
Mwisho.