Rais Trump Amtuhumu Obama Kwa Kudukua Simu Yake
Rais
wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa amegundua Rais mstaafu wa nchi
hiyo ambaye ni mtangulizi wake, Barack Obama alikuwa akidukua simu yake
mwezi mmoja kabla ya kuchaguliwa kuliongoza taifa hilo.
Rais Trump ametoa shutuma hizo kupitia ujumbe wake wa Twitter Jumamosi ambapo ameandika kuwa: ‘Makosa
sana! Nimegundua kwamba rais Obama alikuwa akidukua simu yangu katika
ofisi yangu iliyopo Trump Tower kabla ya mimi kupata ushindi.’
Pamoja
na shutuma hizo, Rais Trump hajatoa ushahidi wowote ili kuthibitisha
madai hayo ama hata kusema ni agizo gani la mahakama alilonukuu.
Aidha,
vyombo vya habari Marekani vimetoa ripoti zinazoeleza kuwa shirika la
kijasusi la FBI liliomba agizo la kuwachunguza maafisa wa karibu wa Rais
Trump kutoka kwa shirika la kigeni la kijasusi Fisa kubaini iwapo
wamekuwa wakiwasiliana na maafisa wa Urusi.
Pamoja na kwamba agizo hilo lilikataliwa lakini baadaye likakubaliwa mwezi Oktoba kulingana na ripoti hizo za vyombo vya habari.