MKOA WA MARA WAPOKEA MBOLEA YA RUZUKU;

 

Musoma

Kutokana na mvua kuendelea kunyesha  katika baadhi ya maeneo nchini Mkoa wa Mara wapokea mbolea ya ruzuku iliyopokelewa na afisa kilimo mkoa wa Mara
 kutoka kwa Tanzania fertilizer company(TFC) ambao ni wakala wa serikali kwa niaba ya katibu tawala wa mkoa kwani yeye ndie katibu wa pembejeo za mkoa  na kukabidhiwa kwa wakala mkuu wa  TFC  wa mkoa anaejulikana kama PONA yeye ni kituo
Akipokea mbolea hizo za kukuzia aina ya urea ambazo ni tani 100 zenye ujazo wa kilogram 50 kwa kila mfuko  mbele ya waandishi wa habari wa mkoa wa Mara ndugu Denis Nyakisinda alisema kuwa kutokana na kuwepo kwa upungufu wa chakula serikali imeamua  kuwahisha mbolea hizi ili wananchi wa mkoa wa Mara waweze kulima kwa wakati  katika kipindi hiki cha mvua za vuli kwa kuwa kuna baadhi ya wakulima wamekwisha panda mazao yao.

Afisa kilimo huyo ambae alikuwa ameongozana na baadhi ya watendaji akiwemo kaimu katibu tawala mkoa bi AnastaziaMajale  na mratibu wa pembejeo mkoa ndugu Kelvin Ruge akiwepo na wakala wa Tanzania fertirizer company (TFC) wa mkoa ambae ni pona,afisa huyo  alisema kuwa elimu ipo na  tayari maafisa ugani walioko katika kata wameishatoa elimu kwa baadhi ya  wakulima .
Nae meneja wa Tanzania Fertilizer Company wa kanda ndugu David Anyambalile Mwakililialisema jumla ya   Mawakala watatu ambao ndio wanaotambuliwa na serikali katika kusambaza pembejeo hizi nao ni  Masito Agrovet ambae  yeye atasambaza mbolea katika wilaya za Serengeti,Musoma vijijini na Butiama na wakala Bitus yeye atasambaza  Tarime mji ,Tarime vijijini nae Lucas Agrovet     anasambaza Bunda na Rorya  awahamasisha mawakala wachangamkie fursa waweze kuchukua kwa wakati iliwaweze kuwasambazia wakulima kwa wakati na kuhudumia  wakulima , na bei kwa mawakala hawa haitazidi elfu arobaini kushuka chini kwa kuwa ni mboea ya ruzuku ukilinganisha bei kwa wauzaji  wa maduka ya pembejeo ambao wanauza kwa kiasi cha shilling elfu sabini (70,000).

Aliongeza kwa kusema kuwa bei ya mbolea hizi za ruzuku bei tayari ilishapangwa na kila halmashauri kulingana na umbali wa kila wilaya na itategemea na umbali husika kiusafiri.

Akithibitisha upokeaji huo mkurugenzi wa PONA agrovet ambae ndie wakala mkuu mwakilishi wa Tanzania fertilizer Company (TFC) wa mkoa wa Mara ndugu Obidient Kasaizi akili kwa kupokea jumla ya mifuko elfu mbili (2000)ya mbolea ya ruzuku ya serikali aina ya urea kutoka kwa afisa kilimo wa mkoa wa Mara ambae amepokea kutoka kwa meneja wa kanda wa TFC  ambazo ni tani zipatazo 100.    
Nae mratibu wa pembejeo mkoa ndugu Kelvin Ruge alifafanua kuwa katika mkoa wetu kuna halmashauri 9 lakini  ambazo zimepata mgao huu ni halmashauri ni saba (7)ambapo  Tarime dc wakulima 100 tu kutokana na kutokuwepo kwa skimu ya  umwagiliaji nao Tarime mji kuna wakulima 300,Serengeti 350 ,Rorya 350,Musoma dc na Bunda wakulima 300 kwa kuwa kuna miundo mbinu iliyojengwa na serikali iliyotambulika na inafanya kazi.
Na Jovina Massano, MUSOMA
Powered by Blogger.