SEKTA YA UVUVI IANGALIWE, TANZANIA


Image result for picha za uvuvi
SEKTA YA UVUVI IANGALIWE TANZANIA ILIKUKUZA UCHUMI WA NCHI.
Na mwandishi wetu; Ada Ouko,Musoma.
 
MCHANGO wa sekta ya uvuvi katika pato la Taifa kwa mwaka 2015 ulikuwa ni asilimia 2.5 lakini takwimu zinaonesha kuwa katika mwaka huo sekta hiyo iliingizia serikali mapato ya shilingi bilioni 12.9 kutokana na kusafirisha nje ya nchi kiasi cha tani 40,540.95 za samaki na mazao ya uvuvi.
 
Pia kati ya tani hizo ziwa victoria lilichangia zaidi ya tani 29,000 na kuingizia serikali zaidi ya shilingi bilioni 11.3 ambayo ni asilimia 87.6 pato linalotokana na sekta ya uvuvi katika kipindi cha mwaka 2015.
 
Hayo yalielezwa juzi na katibu mkuu wizara ya kilimo,mifugo na uvuvi nchini Yohana Budeba wakati alipokua akisoma hotuba yake na kufanya ufunguzi wa mkutano wa kuwasilisha ripoti ya sensa ya uvuvi(frame Survey) ya mwaka 2016 mbele ya wadau wa sekta hiyo kutoka mikoa ya kanda ya ziwa victoria.
 
‘’Ni ukweli ulio wazi kwamba maendeleo ya wananchi katika Nyanja za kiuchumi na kijamii yamekuwa yakitegemea sana shughuli za uvuvi katika halmashauri hizi, ni katika muktadha huo,serikali kupitia idara za maendeleo ya uvuvi na ufugaji wa viumbe katika maji imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa uvuvi katika ziwa victoria unakuwa endelevu na wa manufaa zaidi’’alisema.
 
Budeba alisema miongoni mwa madhumuni ya sensa hiyo ni kupata takwimu zinazohusiana na nguvu ya uvuvi iliyopo katika mavuvi mbalimbali sambamba na hilo kupata idadi ya mialo,idadi ya wavuvi,idadi ya aina ya vyombo vya uvuvi  idadi na aina ya zana za uvuvi, na miundombinu iliyopo katika mialo husika.
 
Kwa kuzingatia hilo alisema ulinganisho wa takwimu za sensa za uvuvi  zilizotangulia na sense ya sasa unaonesha ongezeko kubwa la idadi ya wavuvi,vyombo na zana haramu wakati rasilimali imekuwa ikipungua.
 
‘’Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka 2014 idadi ya wavuvi ilikuwa 103,540 lakini sensa ya uvuvi iliyofanyika mwezi septemba 2016 idadi ya wavuvi waliopo imefikia 109,397 ambalo  ni sawa na ongezeko la asilimia 5.7 vilevile idadi ya vyombo imeongezeka kutoka 29,154 vilivyopatikana katika sense iliyofanyika mwaka 2014 na kufikia 31,773 katika sensa ya mwaka 2016 sawa na ongezeko la asilimia 29’’alisema Budeba.
 
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa idara ya maendeleo ya uvuvi Magese Emmanueli aliwataka maafisa uvuvi kutoka halmashauri za wilaya mbalimbali za mikoa ya kanda ya ziwa kuzingatia sharia no.22 ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2009 vizuri kwani uvivi haramu ukitokea katika maeneo yao afisa husika atawajibika kwa mujibu wa sharia hiyo.
 
Naye afisa uvuvi katika manispaa ya Musoma Joseph Msuya alisema serikali iunde chombo maalumu(fire patrol) na kutoa bajeti kwa ajili ya kuwakamata wavuvi haramu sambamba na hilo asilimia 15 ya mapato yatokanayo na BMU irudishwe kuboresha maslahi ya kamati ya ulinzi na usalama wa ziwa victoria.
Powered by Blogger.