Mama Graca Machel apokea ripoti ya utafiti wa watoto walio nje ya mfumo wa shule,MUSOMA MKOANI MARA
|
Mke wa aliyekuwa rais wa Msumbiji, Samora Machel na rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela Graca Machel leo ameanza Ziara ya kikazi ya siku tatu katika Mkoa wa Mara ambapo amepokea taarifa ya utafiti wa mradi wa watoto walio nje ya mfumo wa shule kwa sababu mbalimbali ujulikanao kama 'out of school project'. Mradi huo unatekelezwa na Mara Alliance kwa kushirikina na Graca Machel Trust(GMT) na Serikali ya Mkoa wa Mara.
Askofu wa Jimbo la Roman Katoliki la Musoma Michael Msonganzila akimpokea Mama Graca Machel ambaye amewasili mjini
Musoma Mkoani Mara leo kwa zira ya siku
tatu .
|
Baadhi ya wadau akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Butiama Anna-rose
Nyamubi wakimsikiliza Mama Mama Machel
|
Askofu Msonganzila akitoa taarifa fupi kuhusu kuhusu
mradi watoto walio nje ya mfumo wa shule kwa Mama Machel
|