Mama Wema Sepetu akamatwa na Polisi
Mama
mzazi wa Wema Sepetu, Mariam jana alikamatwa na Polisi jijini Dar es
Salaam akituhumiwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyiffu kutoka kwa
mfanyabiashara, Alex Msama.
Kwa
mijibu wa gazeti la Mwananchi, Mariam alikamatwa majira ya saa nne
asubuhi na kufikishwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay jana ambapo
alifunguliwa jalada la kesi inayomkabili.
Baadaye aliachiwa kwa dhamana saa 12 jioni baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili.
Inadaiwa
kuwa chanzo ni kuwa, Mariam alikubali kumuuzia Msama nyumba iliyopo
Sinza, Dar es Salaam baada ya benki ya TIB kutaka kuipiga mnanda
kufuatia mama Wema Sepetu kumdhamini mtu katika benki hiyo ambaye
hakurejesha mkopo wake.
Kwa
sababu Msama hakuwa na fedha ya kutosha kwa wakati huo, aliendelea
kutafuta fedha katika benki na wakati huohuo akimpa Mariam fedha kidogo
ambazo zilifikia TZS milioni 14.
Mariam
baada ya kuona mchakato wa Msama unachelewa, aliuza nyumba ile kwa mtu
mwingine bila kumtaarifa Msama aliyekuwa tayari amechukua fedha zake.
Aidha,
jana wakati wa mahojiano Kituo cha Polisi, Mariam alikiri kupewa TZS
milioni 8 ambazo zipo kimaandishi na kusema hatambui fedha nyingine
zaidi.
Msama alipoulizwa kuhusu kumshtaki Mariam alikiri na kusema kuwa yeye anataka kulipwa fedha zake zote.
Kwa
upande wake Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu alithibitisha
kushtakiwa kwa kada huyo na kusema aliandika maelezo ya awali kuhusu
suala hilo na kuachiwa.