ZLATAN AFUNGIWA MECHI TATU, PIA ATAIKOSA ILE DHIDI YA CHELSEA
ZLATAN AFUNGIWA MECHI TATU, PIA ATAIKOSA ILE DHIDI YA CHELSEA
Mshambuliaji mkongwe wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic amefungiwa mechi tatu ikiwemo dhidi ya Chelsea katika Kombe la FA.
FA imemfungia Zlatan baada ya kubainika alimtwanga “kipepsi” beki Tyrone Mings wa Bournemouth.
Beki huyo anatarajia pia kupewa adhabu kali zaidi kwa kumkanyaga Zlatan kichwani kwa makusudi.
MECHI ATAKAZOZIKOSA ZLATAN BAADA YA KUFUNGIWA MECHI TATU KWA KUPIGA KIWIKO
Machi13: Chelsea (UGENINI) FA Cup
Machi 19: Middlesbrough (UGENINI) PL
Aprili Mosi: West Brom (NYUMBANI) PL