WKATI DAR SEASON IKIENDELEA HUKO SHINYANGA ASKARI POLISI AFUKUZWA KAZI KWA DAWA ZA KULEVYA SHINYANGA,WENGINE 33 WANASWA
Jeshi
la polisi mkoa wa Shinyanga limemfukuza kazi askari polisi namba F 9899
PC Hassan Kavindi kwa kujihusisha na dawa za kulevya.
Askari huyo amefukuzwa kazi kwa fedheha kutokana na kukosa uadilifu wakati wa vita dhidi ya dawa za kulevya.
Kamanda wa polisi mkoa huo Muliro Jumanne Murilo ametoa taarifa kwa
vyombo vya habari asubuhi leo asubuhi Jumatatu Februari 13,2017 na
kwamba watu wengine 33 wamekamatwa kwa kusafirisha,kuuza na kutumia dawa
za kulevya.
Amesema watuhumiwa hao 33 wamekamatwa wakati wa operesheni kali ya
kuzuia na kupambana na dawa za kulevya ya wiki mbili iliyoanza Januari
30,2017 ambayo wiki ya kwanza walijikita katika kuzifuatilia kwa siri za
umakini wa hali ya juu taarifa zote za kiintelijensia zinazohusiana na
dawa za kulevya.
Amesema baada ya kuzichuja vizuri taarifa hizo kwa lengo la kuepuka
ubambikizaji wa kesi walifanya operesheni kwa vitendo kwa upekuzi na
ukamataji wa watuhumiwa kuanzia Februari 6,2017.
“Tulikamata gramu 480 za heroine na cocaine,bangi kilo 81,kete za bangi
1,370,misokoto 1,230 ya bangi,mirungi kilo 3 na gramu 1,027 pamoja na
vifaa saidizi vya kujidungia dawa za kulevya ikiwemo sindano na bomba za
sindano 8 zenye ujazo wa CC 0.5”,ameeleza Muliro.