28 wapoteza maisha kwa ajli ya barabarani 2016 Tarime Rorya
TARIME;
Jumla ya ajali zimetokea Kwa mwaka 2016 na kusababisha vifo vya watu 28 katika mkoa wa kipolisi Tarime na Rorya.
Katika kipindi hicho 28 walijeruhiwa huku 44 walipata
ajali wakajeruhiwa vibaya kutokana na Taarifa zilizoripotiwa katika
jeshi la Polisi kitengo cha usalama Barabarani.
Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa polisi Mkoa wa
Kipolisi Tarime Rorya Andrew Satta katika kuhitimisha mafunzo
ya usalama barabarani kwa madereva wa pikipiki Thomas Mapuli alisema
jeshi hill limepata mafakio kwa elimu inayotolewa.
Jumla ya madereba pikipiki 600 wamepatiwa mafunzo katika
wilaya ya Tarime ambapo wamertakiwa kutumia mafunzo hayo katika
kupunguza ajali zinazotokea mara kwa mara.
Mapuli alibainisha takwimu hizo alieleza mikakati ya
jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kuwa ni kuhakikisha
wanamaliza tatizo la ajali za barabarani.
"Katika mwaka huu wa 2017 lengo letu ni kumaliza kabisa
ajali za barabarani na ndiyo maana tunatoa elimu hizi ili mzitumie
wakati mnapokuwa mkiendesha vyombo vya moto," alisema Mapuli.
Faustin Matina ambaye ni Mkuu wa chuo cha udereva Wide
Institute chenye makao makuu mkoani Kilimanjaro alisema mafunzo hayo
yanawalengo mwananchi wote huhu akiwasihi waendesha vyombo vya
moto kufuata sheria za usalama Barabarani.
"Hatuna ubaguzi katika utoajimafunzo hayo, maana hata
waenda kwa MIGUU nap wanatakiwa kufahamu shetia za kutumia barabara, ili
wasikutwe na madhara ya kupata na ajali," alisema Matina.
Akifunga Rasmi Mafunzo hayo Mkuu wa wilaya ya Tarime
Glorius Luoga liwataka madereva hao kusaidia serikali katika suala zima
la ulinzi na usalama kwani wao ni wengi na wanafika sehemu mbalimbali
huku wakisagirisha abiria tofauti wakiwapo waharifu.
"Nanyie mlioko humu ambao ni waharifu achenii tabia hiyo
pia msaidie kuwa watoa taarifa kwenye vyomba vya usalama kuhusu waharifu
pale mnapogundua kuwa abiria uliyembeba siyo mzuri kiusalama," alisema
Luoga.