WANAUME WATAKIWA KUTOA UHURU KWA WAKE WAO

 NA MAKALI BLOG##SIPICHA YA TUKIO HALISI;wanandoa hao wakiwa na watoto wao pichani.
 wanandoa hao wakiwa na watoto wao pichani.
Wanaume  Wametakiwa  kuwapa uhuru wake wa kwa kuachanana na mfumo dume
ili  waweze  kuingia  kwenye  biashara  kwa  lengo  la kukuza  kipato cha familia  na kuondokana  na utegemezi  unaowafanya  washindwe  kujitegemea kimapato.
Kauli  hiyo  imetolewa  na wanakikundi cha  kuweka  na kukopa cha Umoja  Samaritani  katika Maji wa Tarime wakati  wa kufunga  mzunguko wa kuweka  akiba  na kukopa.
Wanawake  hao  wamesema, wanaume zao hawataki  kuwaruhusu  kufanya  biashara  kwa kudai kuwa  watawadharau baada  ya  kupata mafanikio  ya kifedha, hivyo kuwataka kuachana na mfumo dume kuwapa fursa  kwa akina mama hao kufanya biashara ili  kukuza  pato la familia litakalochangia  kuleta maendeleo ya familia  zao na kuwapunguzia wanaume mizogo  waume.
Mtendaji wa mtaa wa Samaritani Halmashauri ya mji wa Tarime Anna Alphonce  anamewataka akina baba ambao wamekuwa wakikimbia familia zao kwa sababu ya ugumu wa maisha, kutofanya  hivyo  bali  washirikiane  na wake  zao  kwa  kujiunga  na  vikundi vya  kuweka na kukopa  ambavyo  vimekuwa  Mwokozi  wa  familia nyingi.
Kwa upande  wake Mwenyekiti wa Mtaa Samaritani Steven Edward amesema Serikali  ina  mikakati ya kuhakikisha kuwa inasaidia vikundi vya akina Mama na vijana ambavyo  vimeonyesha  uwezo  wa  kusimamia  vizuri  mitaji  yao  kwa  lengo la kuwaongezea  mitaji  hiyo  ili  waweze  kufikia  malengo  yao  yakuboresha  maisha  ya familia  zao  kiuchumi.
Aidha Katibu wa kikundi hicho  Elias Amos amesema, mpaka sasa kikundi  hicho kinajumla ya shilingi Million tatu ambazo wanaendelea kukopeshana ili kujikwamua kiuchumi tangu  kikundi  hicho  kianzishwe  mwaka 2016.
Mwisho
Powered by Blogger.