VETERANS FC YAICHAPA NYAMISANGURA 4-2 CCM CUP
NYAMISANGURA FC imekubali kipigo cha mabao 4-2kutoka kwa
VETERANS FC kwenye mchezo wa nusu fainali ya kombe la CCM uliofanyika
katika Uwanja wa Serengeti mjini hapa.
VETERANS ilipata ushindiw huo kwa mikwaju ya penati baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika dakika 90 za kawaida.
Bao La Nyamisangura lilifungwa na Stanphod Clement
katika dakika ya 43 ya kipindi cha Kwanza huku, lile la Veterans
likiwekwa kimiani na Mughusuhi Maganya dakika ya 74 ya kipindi
cha pili.
Matokeo yaliufanya mchezo huo kuwa wa kasi kwa timu
zote kushambuliana kwa kiwango cha juu lakini zikishindwa kuzifikia
nyavu za wapinzani wa.
Kocha wa Veterans FC, Jumanne Kez alisema mchezo huo
ulikuwa mgumu lakini tulijipa moyo tukaongeza bidii tukashinda baada
ya kuingia kwenye mikwaju ya penati.
"Wenzetu hawakuwa wa kubeza kwani kama isingelikuwa
wake fiti tungeweza kuwafunga kwenye dakika 90 za kawaida lakini
ilishindikana hadi matuta,"alisema Kez.
Aliongeza kuwa katika mchezo wa fainali wanotegemea
kukutana na Tarime Amani FC wajiandae kpokea kipigo na mwandaaji
awaandalie huyo ng'ombe kwa kuwa njia ni nyeupe kuwa washindi
wa kombe la CCM.
Kocha wa Nyamisangura FC, Salumu Maule alikubali matokeo
na kusema kuwa mechi ilikuwa nzuri licha ya wao kupoteza mchezo
huo katika hatua ya mwisho.
"Tumekubali matokeo kwani mechi ilikuwa Nzuri Wenzetu
wameweza kupata nafasi na kututumia vizuri katika Hatua ya penati,
"alisema Maule.
MWISHO.