ZOEZI LAKUANDIKISHA VITAMBULISHO KWA WATUMISHI LAKAMILIKA
Zoezi la uandikishaji wa vitambulisho kwa watumishi wa serikali wa mkoa
wa Mara limekamilika, ambapoJumla ya watumishi 13491 wa mkoa wa Mara watapatiwa
vitambulisho vya Taifa vya National Identification Authority(NIDA) kwa awamu ya
kwanza ili kuwasaidia watumishi kufanya
kazi kwa amani kama raia halali wa Tanzania .
Akizumguza wakati wa kukabidhi vitambulisho hivyo kwa
viongozi wa mkoa wa Mara ,makabidhiano ambayo yamefanika katika Ofisi ya Mkuu
wa Mkoa wa Mara,Afisa msajili wa vitambulisho hivyo Mkoa wa Mara,Ohana G.Ngotolainyo
alisema
kuwa jumla ya watumishi 22992 wa mkoa wa Mara walisajiliwa, kwa ajili
ya kutengenezewa vitambulisho vya taifa,lakini waliofanikiwa kutengenezewa vitambulisho
hivyo ni watumishi 21887, na watumishi
550 hawakutengenezewa vitambulisho kutokana na sababu mbalimbali,ikiwepo
ugonjwa,masomo na likizo.
Ngotolainyo alibainisha kuwa zoezi la uandikishaji kwa watumishi wa mkoa wa Mara lilianza octoba
3 mwaka jana na kumaliza octoba 31 mwaka jana katika Wilaya zote za mkoa, na
kwamba hadi sasa wamefanikiwa kugawa
vitambulisho 13491 kwa awamu ya kwanza,na watamalizia kwa awamu ya pili ambapo watumishi 8396 watapatiwa vitambulisho vyao
Aliainisha idadi
kamili ya watumishi watakaopata vitambulisho hivyo kwa kila wilaya,ambapo kwa wilaya
ya Bunda ni watumishi 3309,Rorya ni watumishi 1638 ,Butiama ni watumishi 1667,
Musoma mjini na musoma vijijini ni watumishi 2569,Tarime ni watumishi 2449 na
Serengeti ni watumishi 1859 ambao watapewa
vitambulisho hivyo.
Alizitaja baadhi ya changamoto walizokumbana nazo wakati wa
uandikishaji wa vitambulisho hivyo kuwa ni pamoja na ukosefu wa magari kwa
ajili ya usafiri kufika katika maeneo ya
Mkoa wa Mara,ukosefu wa Ofisi ambazo zina ulinzi wa kuweza kusaidia vifaa
walivyonavyo kuwa salama,na aliiomba Ofisi ya Mkoa wa Mara kuwaandalia mazingira mazuri ya Ofisi na
usafiri wa kutosha watakapo anza zoezi la uandikishaji kwa wananchi mapema mwezi machi mwaka huu.
Mara baada ya kukabidhiwa kitambulisho chake kwa niaba ya
watumishi wote wa Mkoa wa Mara,Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk Charles Mlingwa
aliwashukuru kwa kukamilisha zoezi hilo kwa watumishi wa serikali ,kwani zoezi lilifanyika kwa
weledi wa hali ya juu,pia ametoa wito kwa waandikishaji hao kuhakikisha
wanakuwa makini katika kuwaandikishaji wananchi, ili isitokee mtu ambaye si
raia wa Tanzania akapata kitambulisho.
“hakikisheni wasio raia
hawapewi kitambulisho na sisi hii ndio fursa ya kuwatambua raia na asiye
raia,na itatusaidia hata katika uchaguzi wa viongozi wa mitaa 2019,na ikitokea
mtu ambaye si raia akapata kitambulisho na tukamgundua sisi tutamnyanganya hata
kama ni mtumishi”alisema Mkuu huyo.
Aidha mkuu huyo alisema kuwa atajitahidi kuhakikisha suala
la ulinzi na usalama wa vifaa vya waandikishaji hao vinakuwa katika usalama kwa
kuviagiza vyombo vya ulinzi na usalama,vinasimamia
kikamilifu hadi mwisho wa zoezi la uandikishaji bila kuleta shida yoyote.
Nae Kamishna msaidizi
wa jeshi la polisi mkoa wa Mara ACP Simon Haule alisema kuwa
wanaishukuru serikali kwa kuwapatia vitambulishi hivyo ambayo vinawatambulisha
kama raia halali wa Tanzania na kuwa wataendelea kutoa ushirikiano kwa upande wa ulinzi na usalama wakati zoezi
la uandikishaji litakapo kuwa linaendelea.