Polisi aua mwenzake kwa Kumpiga Risasi na Kisha na Yeye Kujiua
Polisi
amemuua mwenzake kwa kumpiga risasi usiku wa kuamkia leo na yeye
amejiua baada kutazama mechi ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya kati ya
Manchester City na Monaco.
Kabla
ya polisi huyo, Konstebo Constable Patrick Kihagi kujiua kwa kujipiga
risasi kichwani, alimjeruhi polisi mwingine kwa kumpiga risasi begani.
Polisi aliyekufa ametajwa kwa jina la Konstebo James Makokha, na kabla ya kifo alikuwa akifanya kazi Jogoo House.
Inadaiwa kuwa Makokha alipigwa risasi wakati akitaka kumaliza ubishani kati ya Kihagi na Ng’etich.
Kabla
ya tukio hilo saa saba na nusu usiku kwenye eneo la Tassia, Nairobi
nchini Kenya, polisi hao watatu walikuwa baa wakitazama mpira na kisha
wakaanza kubishana, wakatoka nje.
Mashuhuda
wanadai kuwa, walipotoka nje walizidi kubishana, Kihagi akatoa bastola
na kumjeruhi mwenzake, Konstebo Dominic Ng’etich kwa risasi.
Kihagi
alikuwa akifanya kazi katika kituo cha Embakasi, Ng’etich anafanya kazi
kwenye kituo cha polisi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo
Kenyatta.