MAAMUZI YA MAHAKAMA YA RUFAA KATIKA HUKUMU YA KUPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU JIMBO LA BUNDA MJINI.
Wakili wa wakata rufaa, Costantin
Mtalemwa, akitoa ufafanuzi kwa wanahabari baada ya kesi ya rufaa ya
kupinga matokeo jimbo la Bunda Mjini mkoani Mara kuahirishwa na Mahakama
ya Rufaa hii leo Jijini Mwanza.
Mahakama ya
Rufaa nchini imeanza kusikiliza maombi ya rufaa katika kesi ya kupinga
matokeo ya uchaguzi Mkuu 2015 Jimbo la Bunda Mjini mkoani Mara
iliyofunguliwa
na wapiga kura wa jimbo hilo wakipinga ushindi wa mbunge Esther Bulaya.
Wakili wa waleta maombi, Costantin Mutalemwa, amesema hoja
za rufaa hiyo ni za kisheria hivyo mahakama hiyo inaratarajia kupitia hoja zilizowasilishwa
awali ili kujidhirisha ikiwa Mahakama Kuu ilitenda haki baada ya wateja wake
kushindwa katika kesi hiyo.
"Majaji wa
rufani wamesema itapangiwa kusikilizwa, lini hatujui, tutajulishwa.
Waliposhtaki walisema hoja zao ni za kisheria na tuliwachapa kwa hiyo
wameleta rufaa wamesema hoja zao ni za kisheria, tutawachapa vile vile.
Amesema wakili wa mjibu maombi, Tundu Lisu.
Wapiga kura
wanne wa jimbo la Bunda Mjini ambao ni Matwiga
Matwiga, Magambo Masato, Janes Ezekiel na Acetic Malagila walifungua
kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu jimbo la Bunda Mjini uliompa
ushindi Esther Bulaya
(Chadema) dhidi ya Steven Wasira (CCM) wakidai uchaguzi huo uligubikwa
na kasoro kadhaa ikiwemo
mgombea wa CCM kutotaarifiwa kwa maandishi wakati wa majumuisho ya kura
ambapo rufaa hiyo.
Rufaa hiyo
imeahirishwa hadi jumatatu ijayo ambapo Mahakama itatoa uamuzi wake wa
kusikiliza maombi ya walalamikaji na ikiwa kama itasikilizwa Jijini
Mwanza ama Jijini Dar es salaam kama walalamikaji walivyoomba.
Wakili wa mjibu maombi, Tundu Lisu, akiongea na wanahabari
Wakili wa mjibu maombi, Tundu Lisu, akitoka mahakamani
Aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Bunda Mjini (CCM), Steven Wasira (kulia) akitoka mahakamani.
Taswira mahakamani