Waziri Mwakyembe ameeleza wizara yake imebaini kuwepo kwa taasisi na asasi za kiraia zaidi ya 15 zinaendeshwa kinyume
Waziri wa Katiba na sheria Dr Harison Mwakyembe ameleza wizara yake imebaini kuwepo kwa taasisi na asasi za kiraia zaidi ya 15 nchini ambazo zinaendeshwa kinyume na makubaliano ya uanzishwaji wake kwa kutumia mwamvuli kupambana na maambukizi ya virusi vya ukimwi badala yake wanahamasisha vitendo vya mapenzi ya jinsia moja na kuahidi kuzichukulia hatua kali za kisheria
Waziri Mwakyembe amebainisha hayo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na matokeo ya kikao cha 33 wa baraza la haki za binadamu uliofanyika Uswizi ambapo Tanzania iliwakilishwa na Katibu mkuu wa wizara ya hiyo prof SIFUN MCHOME ambapo ulijadili masuala mbalimbali ikiwemo Sheria za ndoa ya mwaka 1971
Amesema kuwa kupitia utafiti wa awali uliofanywa na wizara hiyo umebaini taasisi hizo zimekuwa zikitoa mafunzo katika ngazi ya shule za msingi na sekondari kwa kuandaa majalida na makala mbalimbali katika mikoa 11 ikiwemo Dar es salaam, Dodoma na iringa hivo akamtaka Katibu mkuu wa wizara hiyo kukutana na Makatibu wa wizara husika kujadili suala hilo
Pia ametoa wito kwa wcviongozi mbalimbali wa mkoa wa na wilaya kufatilia na kukemea vitendo hivo ambavyo ni kinyume na katiba ya nchi ya mwaka inayopiga maraufuku ndoa za jinsia moja na kuitaka jamii kuondokana na dhana ya kuwa serikali ya awamu ya tano inawabagua watu kulinagana na maundi yao.