Waziri mkuu Kassim Majaliwa ameendelea kupokea misaada ya waathirika wa tetemeko la ardhi
Waziri mkuu Kassim Majaliwa ameendelea kupokea misaada ya waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani kagera huku akiendelea kuhimiza watu na taasisi kuendelea kujitokeza kutoa misaada zaidi kwani mahitaji bado ni makubwa.
Akipokea misaada hiyo kutoka ubalozi wa japan hapa nchini, makampuni binafsi pamoja na vikundi vya wajasiriamali, waziri mkuu amekabidhiwa misaada ya kibinadamu yenye thaman ya sh million 220 kutoka serikali ya watu wa japan, ambao pia wametoa ahadi ya kukarabati na kujenga shule zote zilizoathirika na tetemeko mkoani kagera.
Wengine waliotoa misaada ni pamoja na kampuni ya madini ya ACACIA ambayo wametoa hundi yenye thamani ya sh million 325, Jumuiya ya wafanyabiashara kariakoo waliotoa vifaa na fedha taslimu vyote vikiwa na dhamani ya sh million sitini, chama cha wakaguzi wa ndani ambao wamekabidhi hundi yenye thamani ya sh million sita, Magereji Tegeta waliotoa fedha taslim million mbili, TBC wamewakilisha hundi ya million 41fedha zilizopatikana kufuatia kampeni walioifanya kupitia vyombo vyake vya habari pamoja na kampuni ya SURA Technoloji waliotoa hundi ya sh million tano.