Watumiaji wengi wa kinywaji cha Chibuku wakiri ni bia ya asili ya kitanzania
Watumiaji
wengi wa bia ya asili ya Chibuku inayotengenezwa na kampuni ya DarBrew
jijini Dar es Salaam wamesema kuwa kinywaji hiki ni bia ya asili ya
kitanzania kwa kuwa kina vionjo vya pombe mbalimbali za asili kutoka
makabila mbalimbali ya Tanzania.
Wamesema
kuwa tofauti ya bia ya Chibuku na pombe hizo ni kwamba imetengenezwa
katika mazingira salama na inamfikia mtumiaji ikiwa imefungwa kwenye
vifaa bora na katika mazingira ya usafi.
Bwana
Simon Mkude,mkazi wa Buguruni akiongea kwa niaba ya wenzake amesema
kuwa hivi sasa watumiaji wengi wa pombe za asili wamegundua ubora wa bia
ya Chibuku na wameanza kuachana na pombe za asili ambazo hazina viwango
na zinauzwa katika mazingira yasiyo salama kwa afya.
Aletas
Matabila mkazi wa Mbezi anasema kuwa yeye na wenzake hivi sasa wameamua
kutumia bia ya Chibuku kwa kuwa licha ya unafuu wa bei inapatikana kwa
gharama nafuu na haivurugi bajeti kama vilivyo vinywaji vingine ambavyo
vinapatikana kwa bei ya juu.
Maria
Lous mkazi wa Kibamba akiongea kwa niaba ya wenzake katika baa ya Mbezi
Inn alisema bia ya Chibuku ni salama kiafya na ina lishe tofauti na
vinywaji vingine ambavyo vinadhoofisha afya za watumiaji wake.
Wakati
wananchi wanaendelea kufurahia ubora wa bia ya Chibuku kampuni
inaendelea na promosheni ya Five Stars ambayo imelenga kuwezesha
wananchi wengi kuelewa ubora wake na kwa jinsi gani kinaleta burudani
sambamba na kupunguza gharama za maisha.
Jina
la Five Star au Nyota Tano kwa Kiswahili katika kampeni hii ambapo kila
nyota inaeleza hali halisia wa bia hii ya asili na ubora wake katika
kuitumia.
Nyota
ya kwanza inaelezea kuwa Bia ya asili ya Chibuku ni Bia ya asili ya
Kiafrika kutokana na jinsi inavyokubalika katika nchi mbalimbali za
Afrika kwa kutumiwa na wengi kama kiburudisho baada ya saa za kazi.
Nyota
ya pili inaelezea vionjo vyenye kiwango cha juu vya bia ya Chibuku
vinavyotokana na mchanganyiko wa malighafi za nafaka zinazotumika
kutengenezea kinywaji hiki
Nyota
ya tatu inaelezea radha inayoridhisha ya bia ya Chibuku ambayo
inapendeza mdomoni na kuleta raha na burudani ya aina yake.
Nyota
ya nne inaelezea ubora wa hali ya juu wa bia ya asili ya Chibuku
kutokana na kutengenezwa kitaalamu na kuwa na viwango vinavyotakiwa vya
ubora usioleta madhara kwa mtumiaji.
Nyota
ya tano inaelezea kuwa bia ya Chibuku ni kwa ajili yetu sote kutokana
na ubora wake inaweza kutumiwa na watu wenye mitindo ya maisha ya aina
mbalimbali pia inapatikana kwenye chupa zenye ujazo wa aina
mbalimbali,hali ambayo inawezesha mtumiaji kukipata kinywaji hiki
kulingana na mfuko wake ulivyo.
Kampeni
ya Five Stars inaendelea kufanyika kwenye vilabu na sehemu nyingi
inapouzwa bia ya Chibuku Super na inazidi kuwafikia wengi na watumiaji
wake kuongezeka , wengi mbali na kuvutiwa na radha nzuri ya bia hii ya
asili wanavutiwa kwa jinsi ilivyofungwa na inavyowafikia watumiaji ikiwa
katika mazingira ya usafi na wengi wanakiri kuwa Chibuku ni bia ya
asili ya kitanzania inayolinda afya za watumiaji wake na kurahisisha
maisha.