Balozi Seif Ali Iddi awachongea Polisi kwa Waziri Nchemba, alitaka kuongeza ulinzi mitaani
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema mipaka ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bado inaendelea kuwa na utulivu kutokana
na kazi kubwa ya u
linzi inayotekelezwa na Jeshi la Polisi inayofanywa kwa kushirikisha vikosi vyengine vya ulinzi.
linzi inayotekelezwa na Jeshi la Polisi inayofanywa kwa kushirikisha vikosi vyengine vya ulinzi.
Balozi
Seif Ali Iddi alisema hayo wakati wa mazungumzo yake na Waziri wa Mambo
ya Ndani wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mwigulu
Lameck Nchemba aliyefika kumsalimia baada ya kuteuliwa na Rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kushika wadhifa huo mazungumzo
yaliyofanyika Vuga Mjini Zanzibar.
Hata
hivyo Balozi Seif alitanabahisha kwamba pamoja na mafanikio hayo ya
ulinzi wa mipaka lakini bado vyombo vya dola vina jukumu la kuwadhibiti
na kuwachukulia hatua za kisheria watu au vikundi vinavyohusika
kusafirisha watu wanaowaingiza nchini kinyume na sheria za Nchi.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar alikumbusha kwamba jukumu la ulinzi wa raia
na mali zao hapa nchini bado litaendelea kusimamiwa na kuwa mikononi
mwa jeshi la Polisi na Wizara ya Mambo ya Ndani.
Balozi
Seif aliiomba Wizara hiyo kupitia Jeshi la Polisi kushirikiana na zaidi
na Viongozi pamoja na Wananchi katika kuimarisha ulinzi ndani ya mitaa
katika dhana nzima ya ulinzi shirikishi.
Akigusia
uwepo wa heshima kwa jeshi la Polisi Nchini Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar ameikumbusha Wizara ya Mambo ya Ndani kurejesha mpango wa
zamani wa ujenzi wa nyumba za makaazi ya askari wake ili kurejesha
heshima ya askari wa Jeshi hilo.
Alisema
wapo askari Polisi katika baadhi ya maeneo nchini wanashindwa
kutekeleza vyema wajibu wao kwa kuhofia kulaumiwa kutokana na ukaribu
wao wa ndani na raia katika maeneo au nyumba wanazoishi na raia hao
kiasi kwamba ukaribu wao unachukuwa nafasi zaidi na kuharibu kazi.
Alilipongeza
Jeshi la Polisi kwa hatua lililochukuwa la kufanya uchunguzi dhidi ya
askari wa usalama Bara barani wa Jeshi hilo aliyetuhumiwa kuchukuwa
rushwa ya fedha taslim kwa raia mmoja wa kigeni baada ya kumkamata
akiendesha gari bila ya kufunga ukanda Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Balozi
Seif alisema kitendo hicho ambacho kilirikodiwa na kusambazwa katika
mitandao ya kijamii kimelitia aibu Jeshi la Polisi Nchini kiasi kwamba
Uongozi wa Jeshi hilo utalazimika kuwa mkali katika kukabiliana na
uzembe kama huo kwa kuwafukuza kazi moja kwa moja wale wanaopatilana na
na makosa ya rushwa.
Mapema
Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania Mh. Mwigulu Lameck Nchemba ameziomba
Taasisi zinazohusika na sheria ya usalama bara barani Zanzibar
kukamilisha Kanuni zilizofanyiwa marekebisho ili ziende sambamba na zile
zilizoanza kutumika Tanzania Bara.
Mh.
Nchemba alisema katika kukabiliana na makosa yanaofanywa na baadhi ya
madereva wazembe bara barani shughuli za ukaguzi unaosimamiwa na jeshi
la Polisi inapaswa ziwe rasmi ili kudhibiti utumiaji mbaya wa bara bara
unayofanywa na baadhi ya madereva.
Waziri
wa Mambo ya Ndani Tanzania alimueleza Balozi Seif kwamba ongezeko kubwa
la vyombo vya moto vya usafiri wa bara barani pamoja na uzembe wa
madereva umeisababishia Serikali kuamua kufanya marekebisho ya sheria
katika kukabiliana na matukio hayo.
Alisema
Kanuni inayosimamiwa na Jeshi la Polisi ya kutoa adhabu ya faini ya
papo kwa papo dhidi ya madereva wanaoendesha vyonvo vya moto bara barani
bila ya kuzingatia sheria na taratibu za bara bara imesaidia kupunguza
makosa na ajali kwenye bara bara nyingi nchini.
Alieleza
kwamba kwa upande mwengine mpango huo wa marekebisho ya Kanuni za
usalama bara barani ulioanza kutumika upande wa Tanzania Bara tayari
umelisaidia Taifa kuongeza mapato yake katika ukusanyaji wa Kodi.
Waziri
Mwigulu Nchemba alifahamisha na kusisitiza kwamba kiu ya Watendaji wa
Wizara yake pamoja na Vikosi vya ulinzi vilivyo chini ya Wizara hiyo ni
kujituma kwa uadilifu ili kufikia matarajio yaliyowekwa na Taifa.