SHILINGI MILION MOJA NA LAKI NNE ZATOLEWA WILAYANI TARIME KUNUSURU KAYA ZILIZOUNGUA NA MOTO



Kutokana na mvua zianazoendelea kunyesha baadhi ya mikoa hapa nchini, Zaidi ya  shilingi millioni moja na laki
Nne zimetolewa  kwa kaya 11 zilizopatwa najanga lakuungua nyumba zao  ambapo  Nyumba 15 katika kitongoji cha Nyabikondo kijiji cha Kewanja kata ya Kembambo Nyamongo Wilayani Tarime mkoani Mara ili wanachi waweze kumalizia ujenzi  wa Nyumba hizo ili kuondokana na adha ya Mvua ambazo zimekuwa nikero kwao.
wananchi hao wakipokea msaada wakukamilisha nyumba zao kujenga ambapo msaada huo umetolewa na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya tarime bw moses misiwa wameishukuru serikali ya wilaya hiyo kwa kuwajali kutokana na adha ambayo wanaipata kwa sasa wakati huu wa mvua zikiendelea kunyesha.  
Moses Misiwa amesema kuwa suala hilo limepatiwa ufumbuzi baada ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya pamoja na mkurugennzi kutemmbelea maeneo hayo na kutoa fedha hizo ili kuwasaidia kumalizia ujenzi wa nyumba zao kuondokanana na adha wanayoipata wakati huu wa mvua.

Kwa upande wake Mtendaji wa Kijiji cha Kewanja Sumun Samson  amesema kuwa suala hilo la nyumba kuungua zenyewe lilichukua takribani siku sita  bila kupatiwa ufumbuzi huku zikungua jumla ya Nyumba 15 katika kaya 11
Ikumbukwe kuwa moto uliokuwa unawake katika vijiji hiyo ulikuwa unahusishwa na imani za kishirikina
Powered by Blogger.