Watuhumiwa wawili kati ya watano wa Ujambazi wamepigwa risasi na polisi na kutiwa mbaroni


 sirronew
Watuhumiwa wawili kati ya watano wa Ujambazi wamepigwa risasi na polisi na kutiwa mbaroni katika eneo la vingunguti jijini Dsm baada ya kutaka kufanya Uporaji wa fedha katika kiwanda kimoja ambapo wengine watatu walifanikiwa kutoroka baada ya kurushiana risasi na polisi waliokuwa wakiwafuatilia.

Kamishna wa Polisi kanda Maalum Dsm Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari amesema majira ya saa tao asbuhi watuhumiwa hao walikuwa wakijipanga kuvamia na kutaka kupora fedha zilizokuwa zinataka kupelekwa Bank ambapo polisi baada ya kuwastukia walianza kurusha risasi na baadae wawili walipigwa risasi za miguu na kukamatwa..
Katika matukio mengine ya uhalifu jeshi hilo limewatia mbaroni watuhumiwa 87 wa matukio ya uhalifu wakiwemo vijana wanaojiita panya road ambao wamekuwa wakiendesha vitendo vya Uvamizi na Unyang’anyi katika baadhi ya maeneo ya jiji la dsm.
Kamanda Siro ametoa onyo kwa wazazi dhidi ya Vijana wao kujitumbukizza katika Uhalifu lakini pia akiwataka wananchi kutoa taarifa za Uhakika ili jeshi hilo lichukue hatua za haraka katika kukabili martukio hayo
Powered by Blogger.