Halmashauri ya Handeni na Kilindi zamaliza mgogoro wa mpaka na Mwekezaji
viongozi wa halamshauri ya wilaya ya Handeni na Kilindi wamefanya ziara ya kwenda kutatua mgogoro wa mpaka wa kijiji cha Gole kilichopo wilayani Handeni na Negelo kilichopo wilayani kilindi.
Ziara hiyo iliofanyika mwishoni mwa wiki Oktoba 8,2016,imefamyika kufuatia kijiji cha Gole kulalamika kuwa kuna muwekezaji anafanya shughuli za kilimo na ufugaji katika eneo la hifadhi ya msitu wa kijiji uliotengwa tangu 2011.
Wakuu wa wilaya ya Handeni na Kilindi sambamba na Wakurugenzi wa wilaya hizo walifika eneo la mgogoro huo wakishirikiana na wataalamu kutoka pande zote mbili,na kusoma ramani iliyotumika kutenganisha mipaka ya wilaya na vijiji.
Mgogoro ulimalizika baada ya wataalamu hao wa mambo ya ramani, kutoa umiliki halali wa eneo aliyopo muwekezaji kuwa ni ndani ya Kijiji cha Gole.Wataalamu hao walieleza kuwa Sheria,taratibu na kanuni zitafuatwa katika kumuondoa muwekezaji huyo katika eneo hilo la hifadhi ili aweze kufanya shughuli zake za kiuchumi katika eneo husika kulingana na mpango bora wa ardhi.
Aidha uongozi uliwataka wataalamu wa pande zote mbili kukaa ndani ya siku kumi kuanisha mipaka inayotenganisha vijiji vya wilaya ya Kilindi na Handeni ili kuondoa utata kwenye vijiji vingine vilivyo na utata.