WATOTO WANNE WAJERUHIWA KWA MOTO NYUMBA ZAFIKA 12 ZILIZOUNGUA NYAMONGO, MBUNGE ATOA MSAADA WA GODORO NA CHAKULA.
PICHA YA MWITA CHACHA AKIWA AMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA NYANGOTO NA MAJERAHA YA MOTO BAADA YA KUUNGUA USIKU WA KUAMKIA SEPTEMBA 13 MWAKA HUU.
Kutokana na hali ya
sintofaamu ambayo inaendelea kutanda katika kitongoji cha Nyabikondo kijiji cha
Kewanja Kata kemambo Nyamongo Wilayani Tarime mkoani Mara baada ya matukio ya
hivi karibuni ya kuungua moto Nyumba 11 na kupelekea hasara kubwa kwa wananchi
bado suala la kuungua nyumba moto linaendelea ambapo kuamkia septemba 13 mwaka
huu watoto wanne wamejeruhiwa kwa moto baada ya nyumba kuungua moto majira ya
saa saba husiku
Aidha watoto hao
walionusurika na moto ni Mwita Chacha wakiwemo watatu wa familia moja ambao ni
,Agustino Karuma,Wankuru Karuma pamoja na Benjamini Karuma ambapo baadhi yao
wamelazwa katika Hospitali ya Nyangoto Nyamongo kwa ajili ya matibabu na hali
zao zinaendelea vizuri
Hali hiyo ya kulipuka
kwa moto bila kujua chanzo ni inazidi kuwaacha vinywa wazi na hofu ya maisha
yao wakazi wa kitongoji cha Nyabikondo Kijiji kewanja Nyamongo Wilayani Tarime
mkoani Mara ambapo wanazidi kuiomba serikali kuingilia kati mara moja ili kubaini chanzo cha moto huo.
Kuruma Zacharia ni mkazi wa kitongoji cha Nyabikondo kijiji
kewanja ambaye ni baba wa familia ya watoto watatu waliojeruhiwa kwa moto
alisem akuwa baada ya matukio ya nyuma ya nyumba kuungua moto aliomba watoto
wake kkujifadi kwa jirani ambapo nyumba ni ya bati kwani nyumba zilizokuwa
zinaungua ni za nyasi lakini ameshanga usiku wa saa saba watoto wakipiga kelele
kuwa moto unachoma nyumba kwa jirani nyumba ambayo ni ya bati.
Zacharia alisema kuwa
baada ya kusikia kelele aliweza kukimbia na kuanza kuokoa watoto hao huku
nyumba ikiwa imetanda moshi sehemu zote na kukimbiza bada majira ya saa nane
usiku watoto hao katika Hospitali ya Nyangoto Nyamongo.
“Moto huu umezidi
kutushangaza jamani sisi wana kitongoji tulidhani nyumba zinazoungua ni za nyasi tu lakini hata za bati zimeweza kuungua
na watoto wangu watatu wamejeruhiwa sana”
alisema Zacharia.
Baada ya matukio hayo ambayompaka
sasa hayajapatiwa ufumbuzi Ofisi ya mbunge wa jimbo la Tarime Vijijini John
Heche kupitia katibu wake Mrimi Zabron
ameweza kuwatembelea wahanga wa matukio
hayo na kutoa msaada wa goro tano pamoja na mchele kilo hamsini huku akitoa
pole kwa niaba ya Mbunge huyo.
“Mbunge anaendelea na
vikao Dodoma lakini nimefika kwa ajili ya kumwakilisha nawapa pole wahanga wa
matukio haya ambayo yanazidi kushangaza jamii poleni sana baada ya wiki mbili
mbunge mwenyewe atafika kwa ajili ya kuwapa pole” alisema Katibu wa Mbunge.
Kemenya Piter Mwera
kwa niaba ya mgaganga mkuu katika Hospitali ya Nyanngoto anadhibitisha
kupokelewa kwa watoto hao huku akisema kuwa mopaka sasa hali yao inaendelea
vizuri
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa kijiji cha Kewanja kata ya Kemambo ambapo matukio hayo yanzidi
kutokea tangu Septemba saba mwaka huu Tanzania Omutima anadhibitisha kutokea
kwa tukio hilo huku akizidi kuwaomba wananchi kuendelea kuchukua taadhali.
Baada ya kutokea kwa
matukio hayo ya kulipuka kwa moto na kuchoma nyumba hovyo mpaka sasa nyumba 12
tayari zimechimwa ambapo kaya saba zimeisha kumbwa na janga hilo huku watoto
wanne wakijeruhiwa kwa moto jamba ambalo limekuwa taaruki katika kitogoji hicho
suala ambalo limepelekea wananchi kutoa
vitu nje huku wakilala nje kwenye miti kwa kuhofia kuungua na moto nakudai kuwa
nyumba zinazoungua ni za nyasi lakini tukio la mwisho ambalo limejeruhi watoto
ilikuwa ni nyumba ya bati na hapa wanananchi wanazidi kutoa kilio kwa serikali
akiwemo diwani wa kata ya Kibasuka Rucy Manyata kuwa nafasi ya viongozi wa dini
ni kubwa katika suala hilo.
Hata hivyo kabla ya
kuungua kwa nyumba ya kumi na mbili mkuu wa wilaya ya Tarime Glorious Luga
aliweza kufika eneo la tukio na kuongea na wanachi huku akisema kuwa endapo
watabaini anayechoma moto huo afikishwe kwenye vyombo vya sheria na siyo
kulipiza kisasi.
NYUMBA ILIYOUNGUA NA KUJERUHI WATOTO WANNE |
KATIBU WA MBUNE MRIMI ZABRON AKISHUDIA MOJA YA NYUMBA ILIUNGUA KWA ,MOTO |