Wafanyabiashara wafunga maduka na kusitisha huduma za Mabasi Songea

Wafanyabiashara wa manispaa ya Songea mkoani Ruvuma leo wamefunga maduka huku huduma ya mabasi  ya nje ya mkoa yakisitisha safari zake,sababu ya mgomo huo ni kuishinikiza serikali ya mkoa wa Ruvuma kusitisha Agizo la kuzuia mabasi makubwa kuingia stendi ya mjini kutoka Songea mkoani Ruvuma.

Channel ten imeshuhudia mabasi yanayofanyasafari zake nje ya mkoa yakiwa yameegeshwa kwenye yadi zake huku abiria wakielezwa sababu ya kusitisha safari kuwa ni mgogoro wa stendi ya mabasi ambapo wamiliki wa mabasi wanapinga agizo la mkuu wa mkoa la kupiga marufuku mabasi kuingia mjini.

Kwa upande wao kampuni ya mabasii ya Super Feo wamesema kuwa wakiwa wanajiandaa kwenda kupakia abiria stendi wakapokea taarifa ya vitisho kuwa kama ataondoa gari yeyote itavunjwa vioo hivyo wakaamua kusitisha huduma.

Wafanyabiashara wa maduka nao wamewaunga mkono wasafirishaji kwa kufunga biashara zao mpka utakapopatikana muafaka wa hatima ya stendi ya mabasi huku wakiwaomba watendaji wa serikali kuwaonea huruma wafanyabiashara ambao  kwa muda mrefu wamekuwa wakiyumbishwa kwa matamko ya viongozi yanayokinzana marumbano yao yanawaumiza.

Katibu wa wafanyabiashara wa stendi Nico Charles amewaambia wafanyabiashara kuwa amepokea taarifa kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Songea yakwamba amewasihi wasafirishaji na wafanyabiashara waendelee kutoa huduma kuhusu madai yao kesho saa mbili asubuhi watazungumza,kufuatia maombi hayo  saa tano asubuhi mabasi yalianza safari ya kuelekea DSM Mbeya na mikoa mingine na maduka nayo yakafunguliwa.
Powered by Blogger.